1 Jun 2009


UMASIKINI AU KUTOKUWA MAARUFU KUNA FAIDA ZAKE,HASA LINAPOKUJA SUALA LA KIFO.UKIENDA KWENYE MSIBA WA TAJIRI NA KUKUTA WATU WANALIA KWA UCHUNGU MKUBWA,USIDHANI NI MAJONZI PEKEE;KUNA WANAOLILIA FEDHA ZA MAREHEMU.PENGINE KUNA UKWELI KWENYE MSEMO KUWA UKIWA TAJIRI AU MTU MAARUFU BASI UTAANDAMWA HADI KABURINI.

HABARI KUTOKA HUKO BONDENI KWA MZEE MANDELA ZINADOKEZA KWAMBA KUNA KIMBEMBE KINAENDELEA KWENYE FAMILIA YA MWANASIASA HUYO MKONGWE BAADA YA MMOJA WA WAJUKUU WAKE KUTUHUMIWA KUUZA HAKI ZA KUTANGAZA MAZISHI YA BABU YAKE NA KUCHIKICHIA ZAIDI YA RANDI ZA KISAUZI MILIONI 3.MJUKUU HUYO MANDLA MANDELA (Pichani KUSHOTO),ANAYETARAJIWA KUWA MRITHI WA KISIASA WA MANDELA,AMEKANUSHA TUHUMA HIZO KWAMBA AMEUZA HAKI ZA MAZISHI YA MANDELA KWA SHIRIKA LA RUNINGA LA SABC.

MANDELA ANA UMRI WA MIAKA 91,LAKINI KAMA TUJUAVYO,NI UCHURO KATIKA JAMII NYINGI ZA KIAFRIKA KUANZA MAANDALIZI YA MAZISHI YA MTU ALIYE HAI HATA KAMA UMRI UMEMTUPA MKONO.WANANDUGU KATIKA FAMILIA HIYO WAMECHUKIZWA SANA NA KITENDO HICHO. LAKINI KWA VILE UMAARUFU NI BI DEAL,INATARAJIWA KUWA PINDI MZEE HUYO AKIFARIKI KILA CHOMBO KIKUBWA CHA HABARI DUNIANI KITAHITAJI KUPATA NAFASI YA KURUSHA TUKIO HILO HEWANI....NA MJUKUU AKAONA LIWALO NA LIWE.

LAKINI SI MARA YA KWANZA KWA MJUKUU HUYO KUMGEUZA BABU YAKE NI MTAJI WA NAMNA FLANI.MWEZI FERBAURI MWAKA HUU ALIRUSHIWA MAKOMBORA YA SHUTUMA PALE ALIPOFANIKIWA "KUMSOMESHA2 BABU YAKE (ALIYEDHOOFIKA KIAFYA) HADI AKAKUBALI KUPANDA JUKWAANI KATIKA KAMPENI ZA MANDLA KUGOMBEA UBUNGE.JAPO BABU MANDELA HAKUWEZA KUHUTUBIA KUTOKANA NA KUWA DHOFUL HALI,TAYARI MJUKUU WAKE ALISHANUFAIKA NA PRESENCE YA MWANASIASA HUYO MKONGWE MWENYE MVUTO

MWEZI JANA,MANDLA ALIZUSHA KIMBEMBE KINGINE BAADA YA KUFANYA NJAMA ZA KUMWONDOSHA BINAMU YAKE KUTOKA KWENYE NYUMBA ANAYOISHI (BINAMU HUYO) ILI BAADAYE AIGEUZE NYUMBA HIYO KUWA KIVUTIO CHA WATALII (KWA VILE INA UHUSIANO NA HISTORIA YA MANDELA,WHICH IN TURN NI DILI LA MAANA).

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube