13 Oct 2009


WAKATI TUNAADHIMISHA KIFO CHA MWASISI WA TAIFA LA TANZANIA,MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE,TUNAPASWA PIA KUTAFAKARI MAMBO KADHAA AMBAYO KWA KIASI KIKUBWA HAYAKUPATA FURSA YA KUJADILIWA WAKATI WA UHAI WA NYERERE,NA KUYAJADILI BAADA YA KIFO CHAKE INAWEZA KUTOA TAFSIRI POTOFU YA UTOVU WA NIDHAMU.

MENGI YAMEONGELEWA KUHUSU MCHANGO WA NYERERE KATIKA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA,NA NDOTO YAKE YA UMOJA ILIYOZAA TAIFA LA TANZANIA KWA KUUNGANA NA ZANZIBAR,PAMOJA NA MCHANGO WA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO YA UHURU KUSINI MWA BARA LA AFRIKA.

BAADHI YA MISINGI ALIYOJENGA NYERERE BADO IPO LICHA YA JITIHADA KUBWA ZA "WANAFUNZI WAKE" KUIBOMOA.WATANZANIA BADO TUNASIFIKA KWA NAMNA TUNAVYOTHAMINI UNDUGU WETU (USHAHIDI UKIWA NENO "NDUGU" KABLA YA MAJINA YETU JAPO WAWAKILISHI WETU BUNGENI WANAITWA WAHESHIMIWA).

KAMA KATUNI YA KIPANYA INAVYOONYESHA HAPO JUU,NYERERE PIA ALITUFANYA TUWE WAPOLE KUPITA KIASI.UPOLE HUO ZAMA ZA CHAMA KIMOJA ULIIMARISHWA NA SHERIA ZILIZOTULAZIMISHA KUAMINI KUWA KIONGOZI YUKO SAHIHI WAKATI WOTE.MADHARA YA IMANI HIYO NI HUJUMA INAYOFANYA NA BAADHI YA WANASIASA KUAHIDI MAMBO WASIYOWEZA KUTEKELEZA LAKINI KWA VILE WATANZANIA NI WAPOLE,NA WANAOAMINI KILA ASEMACHO KIONGOZI,WAMEENDELEA KUTUTAWALA NA SI AJABU WAKAENDELEA KUTUTAWALA ZAIDI.WANAFAHAMU KUWA WANAOWATAWALA HAWANA JEURI YA KUHOJI AHADI ZISIZOTEKELEZEKA ACHIULIA MBALI VITENDO VYA UFISADI VINAVYOFANYWA NA WATEULE WA VIONGOZI HAO.

PAMOJA NA HESHIMA YANGU KUBWA NILIYONAYO KWA BABA WA TAIFA,NALAZIMIKA KUMLAUMU KWA UZAZI NA KULEA TABAKA AMBALO LEO HII TUNALIITA MAFISADI.SIAMINI KABISA KUWA BAADHI YA WANAFUNZI WA MWALIMU WALIKURUPUKA GHAFLA KUWA MATAJIRI KUPINDUKIA HUKUN WAKIKUMBATIA WAGENI NA MARAFIKI ZAO.NAAMINI KUWA WATU HAWA HAWAKUWAHI KUWA WAJAMAA JAPO WALIIMBA NA KUCHEZA UJAMAA MAJUKWAANI WAKIWA NA MWALIMU.

TUMWANGALIE MTU KAMA KINGUNGE NGOMBALE MWIRU.HUYU ALIKUWA SWAHIBA WA MWALIMU NA TULIAMBIWA KUWA DINI YAKE NI UJAMAA.HIVI KWELI KINGUNGE AMEBADILIKA GHAFLA KUWA MTETEZI WA MAFISADI AU ALIKUWA ANAMZUGA TU MWALIMU ZAMA ZA UTAWALA WAKE?

BAADHI YA MADUDU TUNAYOSHUHUDIA LEO YALIANZA ZAMA ZA MWALIMU.KULIKUWA NA KIJITABIA CHA MTU AKIHARIBU HAPA ANAHAMISHIWA PALE,KAMA AMBAVYO AKINA MATTAKA WALIVYOSHINDWA KUIOKOA TRC LAKINI WAKAPELEKWA BIMA.SI KWELI KWAMBA NYERERE HAKUENDEKEZA URAFIKI,MAANA ISINGEKUWA HIVYO BASI ASINGEMPIGIA DEBE MKAPA,RAIS AMBAYE BAADA YA KUTOKA IKULU AMEACHA WATANZANIA WENGI WAKISHANGAA KWA NAMNA ALIVYOTUMIA FURSA HIYO KUJITAJIRISHA (REJEA ISHU YA KIWIRA).

BAADHI YA WACHAMBUZI WA SIASA ZA AFRIKA WANAMTUHUMU MWALIMU KUWA WAKATI ANASTAAFU MWAKA 1985 ALIACHA TAIFA LIKIWA KATIKA HALI MBAYA SANA KIUCHUMI.KUNA WANAODAI KWAMBA UAMUZI WA KUNG'ATUKA UNAOPIGIWA MSTARI KAMA MFANO WA KUIGWA ULIKUWA MATOKEO YA KUKWEPA MAJUKUMU.WAPO WANAOKWENDA MBALI ZAIDI NA KUDAI KWAMBA MWALIMU ALIPASWA KUWAOMBA MSAMAHA WATANZANIA KWA KULIFIKISHA TAIFA LILIPOFIKA WAKATI ANASTAAFU.

HATA SIASA YA UJAMAA NAYO IMEZUA MJADALA KWA BAADHI YA WACHAMBUZI WA SIASA.KUNA WANAOONA KUWA NYERERE ALIKUWA MUUMINI PEKEE WA ITIKADI HIYO HUKU AKIWA AMEZUNGUKWA NA KUNDI LENYE BAADHI YA MATAPELI WA KISIASA WALIOKUWA WANAMUUNGA MKONO JAPO NAFSINI MWAO WALIKUWA NA MAWAZO TOFAUTI.NA MFANO UNAOREJEWA MARA NYINGI NI UAMUZI WA KUUA AZIMIO LA ARUSHA MARA BAADA YA MWALIMU KUTOKA MADARAKANI NA KULETA AZIMIO LA ZANZIBAR.

TATIZO JINGINE LA UJAMAA LIKO KWENYE UKWELI KWAMBA ULIKUWA MITHILI YA JARIBIO,AMBALO KWA KIASI KIKUBWA HALIKUFANIKIWA HADI MWALIMU ANAONDOKA MADARAKANI.KUTOKUFANIKIWA HUKO KULICHANGIWA NA NAMNA UJAMAA ULIVYOSAMBAZWA,AMBAPO MATUMIZI YA NGUVU YALIKUWA JAMBO LA KAWAIDA.REJEA NAMNA OPERESHENI VIJIJI VYA UJAMAA ILIVYOWAATHIRI BAADHI YA WATANZANIA KWA KUONDOLEWA MAHALA WALIPOJIJENGA NA KUPAZOWEA NA KUPELEKWA "UGENINI."HOJA HAPA SI KWAMBA WAZO LA UJAMAA LILIKUWA ZURI AU BAYA BALI KAMA LILIKUWA LINATEKELEZEKA HASA IKIZINGATIWA KWAMBA TANZANIA ILIKUWA TEGEMEZI KIUCHUMI TANGU ILIPOPATA UHURU WAKE 1961.

KUDHANI KWAMBA MAFISADI WALIIBUKA GHAFLA NI KUKWEPA KUDADISI CHANZO CHA TATIZO.MAFISADI WENGI NI TABAKA LILILOIBUKA MIAKA YA MWISHO WA HARAKATI ZA UHURU NA BAADA YA KUPATIKANA UHURU.NI KIKUNDI CHA WARASIMU WALIOTUELEKEZA NAMNA YA KUFANYA JAPO WAO WENYEWE HAWAKUFANYA HIVYO.TABAKA HILI LILIKUWA LINASUBIRI MWALIMU AONDOKE MADARAKANI LIANZE "KUFANYA VITU VYAKE",AND SURE THEY DID!

NYERERE ALIZUNGUKWA NA LUNDO LA WANAFIKI.KISICHO NA HAKIKA NI KAMA ALIFAHAMU UNAFIKI WAO NA KUWAVUMILIA AU WALIMZIDI AKILI.YOTE MAWILI HAYAMTOI LAWAMANI KWA VILE PINDI KIONGOZI ANAPOCHAGUA WASAIDIZI WENYE MAPUNGUFU,AIDHA KWA KUTOJUA AU KWA MAKUSUDI,NI LAZIMA ABEBE LAWAMA KWA UTEUZI MBOVU.

UJAMAA,REGARDLESS YA KUWA ITIKADI YA MAJARIBIO,UNGEWEZA KUZAA MATUNDA MEMA IWAPO UNGEGUSA KILA MTANZANIA PASIPO KUJALI NAFASI YAKE KATIKA JAMII.NI DHAHIRI KUWA LAITI HILO LINGETIMIA BASI TUSINGESHUHUDIA AWAMU YA PILI (BAADA YA NYERERE) IKIENDESHA TAIFA KWA MTINDO WA LAISSEZ FAIRE (BORA LIENDE) NA AWAMU YA TATU IKITUAMINISHA UJIO WA ZAMA ZA UWAZI NA UKWELI HUKU WATU WANAUZIANA MGODI WA KIWIRA KWA BEI YA KISHKAJI.YA UFISADI KILA MMOJA WETU ANAFAHAMU HALI ILIVYO.

KWA VILE MIE NI MKRISTO,NA KWA VILE MILA ZETU ZINAKATAZA KUWASEMA VIBAYA MAREHEMU,BASI NAUNGANA NA WATANZANIA WENZANGU KUMTAKIA MWALIMU PUMZIKO LA MILELE NA MWANGA WA MILELE,APUMZIKE KWA AMANI,AMINA.HATA HIVYO,KAMA SIE WAKATOLIKI TUNAVYOAMINI KUWA ROHO ZA MAREHEMU ZIKO "HAI" TUKIZIKUMBUKA KWA SALA,BILA SHAKA MWALIMU ANAJUTA KUCHAGUA "MARAFIKI" AMBAO BAADA YA KUONDOKA KWAKE WAMEGEUZA TANZANIA KUWA SHMBA LA BIBI,WANACHUMA WATAKAVYO,WANAKWIBA WATAKAVYO,LAKINI KWA VILE ALITUGEYUZA WAPOLE NA WAGUMU KUDAI HAKI ZETU,TUNAENDELEA KUVUMILIA MACHUNGU.

MWISHO,KWA VILE LAWAMA PEKEE HAZIWEZI KUSAIDIA KUTUFIKISHA TUENDAKO,JUST LIKE MAKALA NDEFU ZA KUMBUKUMBU YA MWALIMU ZISIVYOWEZA KUWAKWAMUA WALALAHOI,NI MUHIMU KUITUMIA SIKU HII KUJIULIZA SWALI HILI MUHIMU.JE NYERERE NA WAPIGANIA UHURU WENZAKE WALIPAMBANA NA MKOLONI KWA MINAJILI YA KUMUONDOA MTU MWEUPE NA KUMUWEKA MKOLONI MWEUSI (MAFISADI,et al)?

ANGALAU MKOLONI ALIKUWA NA EXCUSE YA KUTUNYONYA NA KUTUPELEKESHA.HAKUWA MTANZANIA,HAKUWA NA UCHUNGU NA NCHI HII,NA HAKUFIKISHWA ALIPOFIKIA KWA JITIHADA ZA WATANZANIA.LAKINI MAFISADI NI WATANZANIA WENZETU,WANALAZIMIKA KUWA NA UCHUNGU NA NCHI YETU KWA VILE KWA VYOVYOTE VILE BAADHI YA WAATHIRIKA WA UFISADI WAO NI NDUGU ZAO WA MBALI (WA KARIBU WAMESHATENGENEZEWA ULAJI SOMEWHERE).

NJIA BORA YA KUMUENZI MWALIMU NI KUREKEBISHA PALE ALIPOKOSEA (KWA MFANO KUWALEA VIONGOZI WALIOMZUGA KUWA NI WAJAMAA LAKINI WAKAGEUKA MAFISADI MARA BAADA YA KUONDOKA KWAKE) NA KUIANGALIA TANZANIA KAMA NCHI YETU SOTE NA SI YA WATEULE WACHACHE (AMBAO MARA NYINGI HAWATAKI KUSIKIA SAUTI TOFAUTI NA YAO UNLESS IWE NI VIGEREGERE AU MAKOFI YA PONGEZI).TUMUENZI MWALIMU KWA KUKATAA NCHI YETU KUWA SHAMBA LA BIBI HUKU WAWEKEZAJI UCHWARA WAKIJA NA BRIEF CASES TUPU NA KUONDOKA WAKIWA MAMILIONEA.TUKATAE WEZI KAMA WA KAMPUNI YA KAGODA NA MATAPELI KAMA WA RICHMOND,NA UJAMBAZI KAMA WA MEREMETA,TANGOLD,NK KUENDELEA HUKU WAHUSIKA WAKITUPUUZA KWA KUGOMA KUTUELEZA UKWELI.


1 comment:

 1. Enzi za Mwalimu ukimbishia angeku-KAMBONA!
  Nafikiri ndio maana Waheshimiwa wakaribu naye walishastukia mkao wa NDIO Mzee!

  Na labda kulikuwa hakuna ujanja wakati ulishaambiwa ''ZIDUMU FIKRA SAHIHI za MWENYEKITI!''.
  Unafikiri sasa ungezibishiaje baada ya kudai FIKIRA za Mwenyekiti ni SAHIHI?
  :-(

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube