21 Oct 2009


ANDREW CHENGE,ALMAARUF KAMA MZEE WA VIJISENTI ALIPOGONGA NA KUUA,ILIUNDWA TUME MOJA YA CHAP CHAP NA JESHI LA POLISI (SIJUI NI AJALI NAGPI ZINAUNDIWA TUME).HADI LEO HATUJAFAHAMISHWA MATOKEO YA UCHUNGUZI WA TUME HIYO YA "WATAALAM" (JAPO WATAALAM HAOHAO WALIKUWA NA SPIDI YA ROKETI KUBASHIRI CHANZO CHA AJALI YA MWAKYEMBE).

UFISADI KATIKA KITUO KIKUU CHA MABASI CHA UBINGO ULIPELEKEA KUTOLEWA MAAGIZO KWA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI AFANYE UCHUNGUZI.RIPOTI ILIKABIDHIWA KWA MTOA AGIZO LAKINI HADI LEO HAIJAWEKWA HADHARANI.

MABOMU YALILIPUKA MBAGALA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI KADHAA.CHAPCHAP TENA IKAUNDWA TUME YA UCHUNGUZI.IKAWA ASUBUHI,IKAWA USIKU,HATIMAYE RIPOTI IKAKABIDHIWA KWA MTOA MAELEKEZO.KABLA HAJATUJULISHA KILICHOMO KWENYE RIPOTI HIYO MABOMU MENGINE YAKALIPUKA NA KUUA WATOTO WAWILI.LAKINI HADI LEO HATUJAELEZWA SABABU ZA MILIPUKO HIYO JAPO RIPOTI IMESHAKABIDHIWA KWA MHUSIKA.

WAKATI HAYO YAKITOKEA BADO KUNA WINGU KUBWA KUHUSU MAPENDEKEZO YA TUME YA BUNGE YA MWAKYEMBE KUHUSU UJAMBAZI WA RICHMOND.WALIOJIUZULU WAMEACHWA KANA KWAMBA KUJIUZULU KWAO KUMEREJESHA HASARA WALIYOSABABISHA KWA TAIFA (KUMBUKA MGAO WA UMEME UNAOENDELEA NI SEHEMU YA UJAMBAZI HUO WA RICHMOND).LAKINI KAMA KUTUPUUZA,BAADHI YA WALIOHUSISHWA NA UJAMBAZI HUO WANASTAAFU NA MARUPURUPU MANONO.HAPO BADO SIJAGUSIA MDUDU AITWAYE KAGODA.

HIVI BADO MPIGA KURA UNAAMINI KWAMBA MAAMUZI YAKO YA KUIPA KURA CCM MWAKA 2005 YALIKUWA SAHIHI?LAKINI KWA VILE KUFANYA KOSA SI KOSA BALI KULIREJEA,KWANINI USITOE ADHABU YAKO MWENYEWE KWENYE UCHAGUZI MKUU UJAO HAPO MWAKANI?

HATMA YETU IKO MIKONONI MWETU.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube