15 Apr 2010


Nimefarijika sana kuona mahojiano niliyofanya na msanii mahiri wa Bongoflava,Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA,yamechapishwa katika tovuti ya kimataifa ya muziki wa hip-hop,
Hip-Hop-Dance.Net.Pamoja na kuwapatia wasomaji wa blogu hii nafasi ya kuwafahamu Watanzania wenzetu wanaotangaza jina la nchi yetu kwa namna moja au nyingine,dhumuni jingine la mahojiano hayo lilikuwa kutangaza vipaji vinavypatikana nchini kwetu. Japo mahojiano hayo yanaelekea kuzua mjadala mwingine ambao binafsi nautafsiri kama uhuru wa mawazo,ninaishukuru sana tovuti ya Hip-Hop-Dance kwa "kutoa shavu" kwa mahojiano hayo hasa kwa vile Mtanzania mwenzetu mmoja aliamua kuyabania licha ya kumpa ombi ayaweke "kiwanjani" kwake.Again,naamini alifanya hivyo kwa kutumia uhuru wake kuchagua nini kinastahili kuwepo hapo kwake.


Kuhusu suala la elimu ya Mwana FA,ninaomba kumtetea,sio kwa vile nilimhoji,bali kwa sababu naamini anastahili zaidi pongezi kuliko criticism.Naomba niweke wazi kuwa Mwana FA hakuomba mahojiano hayo bali ni mimi niliyemwomba (na namshukuru sana kwa kukubali ombi hilo).Pili,kama alivyosema mwenyewe,mtu haihitaji kuwa na Masters ili aweze kufanya vizuri kwenye bongoflava.Alichukua uamuzi wa kujiendeleza kimasomo kwa vile,kwa mujibu wa maeleoz yake nayoafikiana nayo,fani ya muziki (hasa wetu) haitoi mwamana wa mafanikio katika maisha.Kwa amaan nyingine,alimua kuongeza elimu yake kama hatua ya kimaendeleo mbali na mafanikio yake katika Bongoflava.

Na hata kama angekuwa anadanganya kuhusu elimu yake (which he absolutely doesn't) ingemsaidia nini wakati tayari ana jina kubwa ndani na nje ya nchi yetu?Nadhani baadhi ya wasomaji wanaomtaka "aeleze ukweli" wanapaswa kwanza "kueleza uongo wake" kabla ya kumtaka aseme "ukweli".Nasema hivyo kwa maana kama nasema jina langu ni Evarist,halafu mtu anasema hilo sio jina langu ,basi ni muhimu kwake kuthibitisha jina langu halisi ni nani.

Binafsi,kama mwanafunzi,nimekumbana na zahma kama hiyo ya Mwana FA.Nimekuwa napokea barua pepe na hata SMS za watu wanaoulizia lini namaliza shule.By the way,shule huwa haimalizwi bali mtu anahitimu hatua moja na anaweza kuendelea na hatua nyingine.Kadhalika,katika mfumo wa elimu ya juu hapa,mwanafunzi anaweza kuahirisha kozi yake pale atapoona umuhimu wa kufanya hivyo.In my case,majibu yangu kwa watu wanaoniuliza kistaarabu ni kuwa kuchelewa kumaliza kozi yangu kumesababishwa na A,B,C na kadhalika kisha nawafahamisha hatua niliyofikia.Kwa wale wanaouliza kwa minajili ya "kudhani nauhadaa umma kuhusu elimu yangu" jibu langu huwa jepesi: Mind your own damn business.

Kuna wanaojiuliza inakuwaje mtu atoke IFM na kuja kufanya Masters University of Coventry,nawasihi wafanye utafiti kidogo kwenye mfumo wa elimu ya Uingereza,na pengine hata huko nyumbani.Inawezekana kabisa kupata admission kwenye vyuo vya hapa kwa kigezo cha "sifa linganifu" (equivalent qualifications).Ni kama ambavyo baadhi ya wanafunzi wanavyojiunga na MBA pale Mzumbe au kwingineko baada ya kumaliza masomo ya stashahada kutoka IFM,Nyegezi,Ustawi wa Jamii (pale Sayansi),nk.Kwa kifupi,mifumo mingi ya elimu duniani iko so "accommodating" kwa watu wenye nia ya dhati ya kujiendeleza kitaaluma.

Nimalizie kwa kutoa shukrani kwa wote wanaoendelea kutoa mawazo yao kuhusu mahojiano hayo.Sipingani na mawazo yoyote bali huu ni mchango na mtazamo wangu binafsi (ambao pia unaweza kuwa si sahihi kwa mujibu wa mitizamo mingine).Huo ndio uhuru wa mawazo,alimradi tunatumia lugha za kiungwana na "hatutiani vidole machoni".Kwa Mwana FA,hizi ndio changamoto za Tanzania yetu.

Stay tuned for the next interview na Mtanzania mwingine anayetuwakilisha vilivyo.Can you make a wild guess?Au una pendekezo lolote?

7 comments:

 1. Nimezisoma comments kwa uangalifu sana. Kwa maoni yangu sijaona mtu anayesema MwanaFA anadanganya kuhusu Masters yake ambayo wewe umesema amehitimu. Nahisi Bw Chahali umekuwa too emotional kwa sababu watu wamekuwa na viewpoints zinazokinzana na zako. Wewe umeandika kuwa MwanaFA amefuzu Masters katika Chuo Kikuu cha Coventry. Sasa suala la atamaliza lini kozi hiyo linatoka wapi kama ameshahitimu? Pili, kwa nini asema, na wewe umerudia, kuwa mtu hahitaji kuwa na Masters kufanya muziki mzuri? Huoni kuna mkanganyiko katika statements zilizotolewa? Hakuna anayesema kuwa Masters au PhD inanfanya mtu awe hip hop artist mzuri. Aidha, kuwa na jina kubwa ndani na nje ya Tanzania hukuwazuii watu kuhoji mambo fulani. Pongezi atapewa, lakini criticisms kama ziko valid zitakuwepo. Freedom of expression inaturuhusu tuwe na mawazo tofauti. Nafikiri azichukulie hizo criticisms constructively. Tusitukanane, kukejeliana, au kudhalilishana. Tuwe na amani.

  ReplyDelete
 2. Evarist huwajibiki kumtetea MwanaFA, mwache aeleze his side of the story. Pili, kama unadai kuwa elimu yake ni suala ambalo ni personal, basi mafanikio yake ya muziki ni personal. Kwa nini hili la pili unaruhusu watu kuuliza, lakini la kwanza hutaki? Tatu, mbona elimu yake ya IFM unitaja halafu unazuia watu kutoa maoni kuhusu suala la Masters?
  Ufahamu kuwa kuna baadhi waTanzania waliosoma au wanaosoma Coventry University. Kwa hiyo, inaonekana kuna kitu fulani ndiyo ambacho hakiko wazi wadau wa muziki wanataka kufahamu MwanaFA. Utetezi wako umeleta mkanganyiko zaidi. Aidha, unaonyesha kuwa unataka watu wote watoe pongezi kwa MwanaFA hata pale pasipositahiki.

  ReplyDelete
 3. Safi sana anonymous hapo juu.
  Evarist kuna options kadhaa ambazo ungechukua:
  1) Kutoeleza kabisa kuhusu elimu ya MwanaFA
  2) Kueleza elimu yake na kusema kuwa wadau wasichangie kuhusu suala la elimu yake.
  3) Kutoweka sehemu ya kutoa comments ili tupate maelezo kutoka kwake na kwako.
  Nikukumbushe hata nyumbani mawaziri, wabunge na public figures wanaulizwa kuhusu elimu yao. Kwa hiyo siyo jambo geni sana kwa MwanaFA.
  Mwisho, tumkumbushe MwanaFA kuwa unapokuwa unajulikana, basi issue yako ndogo sana inakuwa a public maatter.
  Otherwise, I wish you the best in your endeavours.

  ReplyDelete
 4. Ndugu Chahali.
  Hutaki watu wachangine maada hapa kwenye blog yako? Mbona lugha yako imekuwa kali sana? Labda wewe ni mmoja wa fans wa MwanaFA na unafikiri baadhi ya comments zinamshusha chini? Mbona sijaona jambo lolote baya?
  Halafu umesahau kitu kimoja anayedai kitu fulani ndiye anatakiwa kuthibitisha kitu hicho (he who alleges must prove). Wewe na MwanaFA ndiyo mnaodai kuwa MwanaFA amehitimu na ana shahada ya uzamili. Sasa iweje wanaouliza wathibitishe wanachotaka kujua?
  Let's be fair jamani.

  ReplyDelete
 5. Samahani waungwana kama nimewakwaza kwa mchango wangu.Kama nilivyosema sipingani na mawazo yoyote,na nawasihi muendelee na michango yenu maridhawa ya mawazo.Karibuni sana.

  ReplyDelete
 6. Ndugu yangu Evarist. Asante sana kwa mahojiano. Nimefurahishwa sana kuona msanii wa nyumbani akijiendeleza kielimu. Naamini kuwa wachangiaji katika mahojiano yako na MwanaFA na hapa wana hoja halali ya kuuliza kuhusu suala la elimu ya msanii huyu. Hii ni kwa sababu suala hili limetajwa. Kama lisingetajwa, basi wasingeuliza. Pili, sijaona mtu aliyetukana wala kutoa kauli mbaya dhidi ya kijana wetu MwanaFA.
  Ningeshauri kuwa kwa sababu mawasiliano siyo tatizo mwandikie msanii huyo kwa barua pepe ya siri (tembelea tovuti yake utapata anuani yake). Akikubali, atakupa maelezo ambayo unaweza kuyaleta kama maelezo ya nyongeza. Vinginevyo, credibility yako kama blogger na MwanaFA vitaingia dosari. Wewe ni mtafiti, fanya mambo kitafiti. Mungu Ibariki Tanzania

  ReplyDelete
 7. duh hii inadhihirisha ni jinsi gani sisi watanzania tunaweza kugeuza maneno .... kifupi ni kwamba jamaa alivyoeleza hataki kuchanganya mziki wake na elimu yake mtu kapick neno huhitaji MSC kufanya mziki mzuri,, Mimi binafsi nipo Coventry Uni na jamaa amemaliza masters yake na alikuwa akifanya na bwana mdogo Jabir na wote baada tu ya kumaliza wamerudi nyumbani kuendeleza gurudumu la maisha, mi sio msemaji wa FA ila hilo nalifaham kwa kuwa wao cozi yao iliisha mapema ingawa tulikuwa tunaintaract kwenye baadhi ya vipindi kwani wao ni MSC na sisi ni MBA ingawa nijuavyo mimi graduation ni mpaka mwezi wa sita nadhanbi kwenye 24th hivi.
  Huo ni mtazamo wangu tu jamani msijenge chuki.....

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube