14 May 2010

Picha kwa Hisani ya SARAH wa Angalia Bongo.

Bila shaka ushaskia msemo wa Kiswahili 'Kufa Kufaana'.Nadhani kwa kimombo ndio tunachoita 'blessing in disguise'.Na ndivyo inavyoelekea kutokea katika sakata la 'ugomvi' kati ya msanii T.I.D na supastaa wa mpira wa kikapu,Mtanzania Hasheem Thabit,anayechezea timu ya Memphis Grizzliers kwenye ligi maarufu ya NBA huko Marekani.Katika pitapita yangu mtandaoni nimekuta habari hiyo imeshadakwa na vyombo vya habari vya kimataifa.Why not wakati Hasheem ni jina kubwa huko Marekani?

Sasa yayumkinika kusema kuwa sakata hilo limemnufaisha T.I.D 'kiaina' kwa vile katika kuripoti habari hiyo jina lake pia limekuwa likitajwa kama inavyoonekana katika habari ifuatayo kwenye mtandao wa kituo cha runinga cha FOX MEMPHIS cha huko Marekani:

MEMPHIS, Tenn. - The agent for Memphis Grizzlies center Hasheem Thabeet has told the team that an alleged incident involving Thabeet and R&B singer T.I.D never took place.


FOX13 Sports Director Matt Stark spoke with Ugo Udezue, Thabeet's agent, by phone Tuesday night, and Mr. Udezue said the allegations that Hasheem had knocked out the singer were completely false.


Udezue acknowledged that Thabeet was in a nightclub last weekend when an altercation broke out, but that the Grizzlies center was in a private section of the club and being protected by three bodyguards at the time, which is the norm for Thabeet when staying in Tanzania. Udezue says his client was immediately removed from the club, and was stunned later to hear the allegations that he had been involved.


Udezue said he believes the singer made the story up as a publicity stunt, and to get his music played on the radio.


Habari hiyo imekamata kasi kwenye mtandao kama inavyoonyesha HAPA.Japo natambua kuwa msanii T.I.D  'ana jina' kiasi chake katika anga za kimataifa,lakini ni dhahiri tukio hili linaweza kuwa limemtangaza zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

I just hope ugomvi huo haukuwa publicity stunt na publicity iliyojitokeza kwa T.I.D ni coincidental tu.Otherwise,mastaa wa kimataifa wataendelea kukutana na zahma kama hizo kwani zinaelekea kuwa na manufaa kwa upande mmoja wa wahusika wa tukio.

Ama kweli kufa kufaana!

3 comments:

  1. yaani hiyo ni zaidi kufa kufaana.....hapo T.I.D ameshinda lottery...na pengine ndicho alichokuwa anatafuta kupata publicity...inakukumbusha enzi za Makumbi Juma-homa ya jiji akiwa na yanga baada ya mechi na kiboko ya vigogo- Reli ya Morogoro enzi hizo!!!!!! walikuwa wakijimwaga kwenye dansi Morogoro Hotel maarufu kwa jina la shimoni....basi miongoni wailiudhurulia alikuwa ni kundi moja na mimi usiku ule...hivyo ili atuonyeshe kwamba amepata nafasi kuwa karibu na super star wa soka...homa ya jiji bila kujua alikuwa amemkanyaga mguu huyu rafiki yetu...na yeye rafiki yetu alitulia kimya huku akiaangaza macho kwetu ili huku akituonyesha kwamba amekanyagwa mguu na Makumbi Juma-Homa ya jiji. Na yeye rafiki kusema amefarijika sana kuapta hiyo fursa angalau kukanyagwa mguu.....

    ReplyDelete
  2. Unfortunately for Thabit (Americanized as 'Thabeet') his fame doesn't go with class.

    T.I.D might be in a wrong but that is not justification of any kind for Thabit,an NBA player to hit him like he did, unless, I should insist 'UNLESS', for self-defence, something didn't appear to be so!

    How many times we have heard him (Thabit) 'misbehaving' badly in KADAMNASI? I don't have time but if I would, I could!

    ReplyDelete
  3. Mbona nasikia kuwa TID ameutafuta ugomvi huu makusudi. Ila sidhani kama hii itamnufasha TID in any monetary terms apart from being known Terribly Infectious Desease(TID) of Africa probably people will think HIV

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.