Picha kwa Hisani ya SARAH wa Angalia Bongo.
Bila shaka ushaskia msemo wa Kiswahili 'Kufa Kufaana'.Nadhani kwa kimombo ndio tunachoita 'blessing in disguise'.Na ndivyo inavyoelekea kutokea katika sakata la 'ugomvi' kati ya msanii T.I.D na supastaa wa mpira wa kikapu,Mtanzania Hasheem Thabit,anayechezea timu ya Memphis Grizzliers kwenye ligi maarufu ya NBA huko Marekani.Katika pitapita yangu mtandaoni nimekuta habari hiyo imeshadakwa na vyombo vya habari vya kimataifa.Why not wakati Hasheem ni jina kubwa huko Marekani?
Sasa yayumkinika kusema kuwa sakata hilo limemnufaisha T.I.D 'kiaina' kwa vile katika kuripoti habari hiyo jina lake pia limekuwa likitajwa kama inavyoonekana katika habari ifuatayo kwenye mtandao wa kituo cha runinga cha FOX MEMPHIS cha huko Marekani:
MEMPHIS, Tenn. - The agent for Memphis Grizzlies center Hasheem Thabeet has told the team that an alleged incident involving Thabeet and R&B singer T.I.D never took place.
FOX13 Sports Director Matt Stark spoke with Ugo Udezue, Thabeet's agent, by phone Tuesday night, and Mr. Udezue said the allegations that Hasheem had knocked out the singer were completely false.
Udezue acknowledged that Thabeet was in a nightclub last weekend when an altercation broke out, but that the Grizzlies center was in a private section of the club and being protected by three bodyguards at the time, which is the norm for Thabeet when staying in Tanzania. Udezue says his client was immediately removed from the club, and was stunned later to hear the allegations that he had been involved.
Udezue said he believes the singer made the story up as a publicity stunt, and to get his music played on the radio.
Habari hiyo imekamata kasi kwenye mtandao kama inavyoonyesha HAPA.Japo natambua kuwa msanii T.I.D 'ana jina' kiasi chake katika anga za kimataifa,lakini ni dhahiri tukio hili linaweza kuwa limemtangaza zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.
I just hope ugomvi huo haukuwa publicity stunt na publicity iliyojitokeza kwa T.I.D ni coincidental tu.Otherwise,mastaa wa kimataifa wataendelea kukutana na zahma kama hizo kwani zinaelekea kuwa na manufaa kwa upande mmoja wa wahusika wa tukio.
Ama kweli kufa kufaana!