19 May 2010


Picha kwa Hisani ya Michuzi

Nyuso zao zinasuta nafsi zao.Lakini hii ndio hali halisi ya Tanzania yetu.Pamoja na madudu yooote yanayoendelea kufanywa na CCM lakini Watanzania wengi wanaendelea kuwa usingizini na kuamini kuwa hakuna maisha pasipo CCM.Ungetarajia tabaka la chini (ambalo ndio mtaji mkubwa wa chama tawala) liwe na hasira ya hali ya juu dhidi ya chama kilichowasaliti kwa kukumbatia wafanyabiashara mafisadi huku hali za walalahoi zikizidi kuwa ngumu.Lakini,sijui ni kurogwa au vipi,tabaka hili la chini linaendeleza ndoa yake na CCM kama picha inavyoonyesha hapo juu na hapa chini (wanapozugwa na Kingunge).

Na ni hawahawa utakawasikia wakilalamika baada ya uchaguzi kuwa ahh viongozi wametusahau,na malalamiko mengine kama hayo.CCM ikiwapuuza inaweza kuwa na sababu za msingi kwani haikuwalazimisha waipende,na 'imejitahidi kuwapa sababu kadhaa za kuichukia' lakini wananchi hawa wameendelea kuwa ving'ang'anizi.Yani ni kama mwanamke anayeteswa na mume lakini anaendelea tu kumg'ang'ania licha ya kufahamu kuwa mapenzi ya mume huyo yamehamia nyumba ndogo.Na mfano huu unaweza kulinganisha na ndoa ya CCM na wakulima na wafanyakazi,ambapo kwa mazingira ya sasa ya 'ndoa' hiyo CCM imehamishia mapenzi kwenye nyumba ndogo ambayo ni wafanyabiashara na mafisadi.

Kaaazi kweli kweli

8 comments:

  1. Waangalie sura zao zilivyo zinaonesha ni watu waliochoka kiafya na inasikitisha kuona bado hawajitambui(hao wamedungwa sindano ya chanjo na CCM) nini wafanye wanaendelea kufanya vitu kwa mazoea wakitegemea CCM itawasaiia na kubadilisha maisha yao kuwa bora! Kamwe CCM haipo tayari kufanya hivyo isipokuwa usawa wa katika vyama vya siasa na uwakilishi Bungeni ndiyo nguzo ya maendeleo ya kweli ya Tanzania yetu ya leo...

    ReplyDelete
  2. Dr Chahali husishangae hao tuu hata huko ughaibuni wapo pia wanafungua matawi ya CCM...Lakini hatujawahi kusikia ama kuona wakenya, wamalawi, wachina, wamarekani, wanigeria,warusi waghana ambao ndiyo wengi kwa idadi huko ughaibuni. Nchi ya Ghana ndiyo raia wake wengi huko UK kuliko nchi zingine za kiafrika, na pia imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kiuchumi na kidemokrasia ya vyama vingi. Kamwe Raia wake hawana huo upuuzi wa kufungua matawi ya vyama tawala vya kisiasa vya nchi zao ughaibuni.

    ReplyDelete
  3. Kichekesho wao wanafungua matawi ughaibuni wakati huo huo hawako entitled kupiga kura wakiwa wanaishi nj ya nchi!!!!

    ReplyDelete
  4. Kaka Chahali nimecheka kweli hii post yako.kweli inasikitisha kuona watu wamechoka namna ile na bado hawa elewi nini wafanye na hata kama wanaelewa basi ndo kama mtu anaye ambiwa huu msitu kuna simba lakini anaingia msituni bila wasiwasi ili hali anajua kuna simba sasa akiliwa sijui atamlaumu nani?. sisemi kama wana akili kama za mbuzi ila matendo yao yapo hivo, mbuzi akiona mbwa kajificha anaenda kuchungulia ili hali anajua mbwa hatomuacha!!

    Mimi nadhani tatizo ni elimu duni walio nayo dhidi ya siasa ambayo inachukulia kutojua kwao kama ngazi ya kuendelea kufanya madudu.Hawa watu bado wapo kwenye doxa World kwa maana hio wachache wanaojua wataendelea kudidimiza wasiojua mpaka hao wasio jua watakupo zinduka which will of course be too late!!!.

    Na hawa wanaitwa vyama pinzani kama wanajijenga mjini tu hawaendi vijijini basi wasahau kuja kushika uongozo wa juu wataishia huko huko kwenye ubunge na udiwani.Vijijini watu wote wanajua CCM tu ndio chama cha kisiasa!! Hawajui vyama vingine ni baadhi tu ya vijiji ambako wanajua.

    Yaani inasikitisha kweli kwani hapa tusiseme sana kuhusu chama bali hata watu wenyewe wanao wachagua unakuta mtu wanaye mchagua sio muwajibikaji ila muhongaji mzuri. Anawahonga mamilioni na wao wanamchagua yule yule sijui wanadhani yule mtu mamilioni yote hayo ana print tu nyumbani kwake?

    Halafu huyohuyo mtu apite waanze kulalamika 'AMETUSAHAU' amewasahau nini wakati mlisha malizana! si kesha wanunua biashara imeishia pale! Sasa huyo walio mchagua atakua yu bize kurudisha mamilioni yake! kweli hii 'ndoa sijui itavunjwa lini!!!! Ivi kwani haiwezekani wale wanao honga wahonge na wasichaguliwe pia? kwanini mtu achaguliwe ili hali anajulikana ni mtoa rushwa?

    ReplyDelete
  5. Rijakis, ni kweli unaweza kuonga na pia mgombea/wagombea wasichaguliwe...Je hao wanafungua matawi ya CCM huko ughaibuni nao hawana Elimu na Exposure!?

    ReplyDelete
  6. ebana kaka ccm mi sioni sababu ya chama hiki watu kukikumbatia hakina maana angalia kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa habari viongozi wangapi wa ccm au ni watu wangapi wanahusika katika ishu ya ufisadi lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa juu yao mimi inaniuma sana kuona watu wanateseka kwa ajili ya gharama kubwa viongozi wanazotumia kwa ziara na mambo mengine yasiyokuwa na msingi hasahasa raisi kikwete najiuliza kila siku ni lini ccm itaanguka?jamani tuamkeni tujaribu na upinzani ccm mpaka lini na umaskini mpaka lini secure tomorrow today

    ReplyDelete
  7. mnashaangaa Uk mwezi uliopita waziri mkuu Pinda alitutembelea tokyo anatuambia tukitaka maendaleo zaidi Japan inabidi tufungue matawi ya CCM kama Uk sasa sijui huko UK mnamaendeleo kiasi gani kutokana na CCM mtufahamishe ili nasi tujue maana hawa wameshindwa kupeleka maendeleo nyumbani Tz wameyaleta huko Uk au ndio nasi tunaonekana wajinga tunadanganyika kirahisi hivyo?
    Kibaya zaidi ziara ya kiserekali na msururu wa watu kama kawa halafu anatuambia upuuzi wa CCM!balaa

    ReplyDelete
  8. Hivi hamjui kama CCM imegeuka kitengo cha biashara tena za ujanjaujanja kwa hiyo watu wengi wanaotaka mafanikioa ya haraka bila jasho ndio kimegeuka kimbilio lao.
    Shauri yenu kalagha bao tulio mbali tumeliwa ndio wanavyosema wenyewe,!!
    kazi si kidogo

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.