31 May 2010


Nafahamu unaweza usinielewe kwenye post hii lakini naomba niweke bayana kuwa niko radhi kutofautiana nawe msomaji wangu mpendwa.Kwa tutakaoafikiana,all I can say is POA.Nimeguswa na habari kuwa jana Makamu wa Rais,Dkt Shein, amezindua mbio za mwenge.Lengo la makala hii ni kuibua mjadala kuhusu suala hili la MWENGE WA UHURU.

Zamani hizo,mwenge ulikuwa na maana kubwa kwa kila mahali ulipopita.Lakini ni dhahiri kwamba mbio za mwenge kwa sasa hazina tofauti na ngonjera kuwa "Tanzania ni nchi ya Kijamaa" au kaulimbiu kwamba "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania Yanawezekana".

Hili dude linalokula mamilioni ya shilingi katika gharama za kununua mafuta ili liendelee kuwaka,sambamba na posho kwa wanaolizungusha nchi nzima lina umuhimu gani kwa sasa?Maana zamani hizo mwenge ulikuwa na madhumuni ya KUMULIKA lakini sote tunafahamu kuwa kwa muda mrefu sasa mwanga wa mwenge huo unamulika vichochoroni tu huku ukishindwa kuwaangazia macho mafisadi wanaotafuna nchi yetu kama mchwa.Natambua kuwa kuna miradi mbalimbali inayozinduliwa wakati wa mbio za mwenge lakini hilo linafanyika hata wakati mwenge umezimika.Kwa maana nyingine,mwenge uwake usiwake bado wananchi wataendelea kujikusanya (pamoja na uchovu wao) kujitafutia maendeleo yao wenyewe.

Tatizo kubwa la sie Waafrika ni kuendeleza "mila na desturi" hata pale zilipopitwa na wakati.Hivi fedha zinazotumika kuzungusha mwenge nchi nzima zinaweza kujenga zahanati,shule na barabara ngapi?Kwa hakika ni nyingi tu.

To cut the story short,mie nina mtizamo kuwa mbio za mwenge zimepitwa na wakati.Naamini kuwa gharama zinazotumika katika mbio za mwenge zinaweza kutumika vizuri zaidi kwenye maeneo mengine ya msingi.Mwenge unakimbizwa kila mwaka lakini umasikini wa Watanzania unazidi kuongezeka (puuza kauli za Mkulo kuwa uchumi unazidi kukua kwani analipwa mshahara kusema 'lolote'),ujambazi ndio usiseme,na mafisadi wanazidi kulindwa na chama tawala.Sasa hili dude linalokula mafuta kama halina akili nzuri bado lina umuhimu kweli kwa mazingira ya Tanzania ya sasa?

Karibu uchangie

1 comment:

  1. The Objectives na Purpose za Mwenge wa Uhuru ni zilezile ambazo the father of the nation Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema wakati wa uzinduzi wa kwanza wa Mwenge wa Uhuru....thanks Evarist kwamba you still remember!

    MWENGE WA UHURU
    First of all Evarist may I let you know kwamba Mwenge wa Uhuru unatumia gharama ndogo sana ambayo you will not imagine....labda pipa mbili tatu za Diesel! Is that an issue for goverment spending??. Halafu pia wale wakimbiza mwenge hawalipwi kwa kazi ya kukimbiza mwenge, ile ni kazi ya kujitolea so they are just being given a subsistance allowance ambayo tena ni below official Govt DSAs

    So if you compare faida ya mwenge na kiasi cha gharama utaona kuwa its nothing! Pia gharama za mwenge huwa zinakuwa covered na serikali yenyewe na hakuna mtu anayechangia gharama hiyo ...if anyone told yo so....amekudanganya! but I agree with you kuwa kuna michango huwa inafanyika kwa kuratibiwa na local gvt authorities na michango hii inapaswa kuwa hiyari sio lazma na kazi ya michango hii huwa inapangwa katika level ya Manicipals na Councils na fedha hizi ndizo zinazotumika katika kufanikisha miradi ambayo Mwenge unazindua na kuweka mawe ya msingi. As you know Mwenge unawafanya viongozi wa LGAs wachacharike sana waweze ku-finance kwasababu pia kupitia miradi hii viongozi wanapimwa na kupewa credit ambapo Wilaya iliyofanya vizuri zaidi katika kanda na kitaifa zinazawadiwa na His Exellence President of Republic siku ya kilele ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele cha wiki ya Taifa ya Vjana. So you can see guy....hela ngapi zinatumika ovyo ovyo you dont complain but you complain at this good thing!

    Mwenge mbali na kutumiwa kama chombo cha kuchochea maendeleo pia it is a tool for advocacy....kila mwaka kuna ujumbe ambao unapelekwa kwa wananchi na only this thing Mwenge ndio am,bao unafika ktk kila angle ya nchi zaidi kitu kingine chochote hata Mass Media!. Kwam mfano ujumbe wa mwaka huu ni mapambano dhidi ya Malaria, HIV/Aids, Madawa ya Kulevya, Rushwa, Ukatili dhidi ya Albino na Wanawake na Uchaguzi Mkuu 2010. kabla ya kuanza mbio kila mdau kutoka katika taasisi inayojihussha na masuala hayo niliyotaja alishirika katika kuwajengea uwezo wakimbiza mwenge hawa wa 5 ili waweze kuelezea masuala hayo kwa ufasaha kwa wananchi which is more effective and cheap compared na the use ya mass media ambayo pia huwa haiwafikii watu wengi....pia machapisho mbalimbali kuhusu masuala hayo , nyimbo n.k huandaliwa. so you can see how effective is this....kwahiyo pamoja na ujumbe huo wa kila mwaka pia zikle core objective Uhuru,Uzaledo, Utu, Amani, Umoja na Mshikamano na part and parcel na mwenge ume-play role kubwa sana katika hili the problen is ....it is not easy ku measure kwa haraka haraka.Na utaona ndio maana ujumbe wa malaria kwa mwaka huu umekuwa mainly sponsored na John Hopkins Foundation ya USA, MOHSW na NMCP, HIV/Aids(PSI, TACAIDS & National Aids Control Program), Rushwa(PCCB) N.K

    Mwenge pia unatumika katika kuhhamasisha kujitolea katika Tanzania na kila mwaka takwimu zinatolewa kwa thamani ya nguvu za kujitolea zinazofanywa na wananchi, mchango wa serikali na wahisani na kwakuwa wale waliofanya vizuri wanakuwa recognised hivyo watu wanajitahidi sasa kufanya vizuri kiasi cha kwamba Umoja wa mataifa katika kuadhimisha miaka 10 tangu mwaka wa kujitolea utangazwe wamemchukua mwenge kama mfano bora wa kuigwa., kiasi cha kwamba katika mwaka huu majirani zetu Msumbiji wame copy na wamezindua rasmi mwenge wao wakati Zimbabwe wapo pia mbioni kwavile walikuja hapa kujifunza.

    Evarist unakumbuka uzinduzi wa mbio za Mwenge mwaka 1991 jinsi ulivyoshiriki kikamilifu na kwa uzalendo mkubwa, thtats how it is man!!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.