10 Jun 2010

Uandishi wa blogu si jambo rahisi kama inavyodhaniwa na wengi.Na ni jambo gumu zaidi kwa akina sie tunaoelemea zaidi katika kuandisha mambo yanayogusa maslahi ya mafisadi na vibaraka wao.Kwa mfano mara kadhaa nimekuwa nikipata comments zenye matusi ya kila aina kutoka kwa baadhi ya wasomaji.Huwa siyachapishi matusi hayo kwa vile naamini wanaotukana wana mtindio wa mawazo na tafakuri.Hoja hujibiwa kwa hoja na wala si matusi.

Ninafahamu matusi hayo yanatoka wapi,na pia natambua kwanini badala ya hoja zangu kujibiwa kwa hoja zao wanakimbilia kutukana.Ni hivi,ukiona mtu anakusema vibaya au kukutukana wakati hujamkosoea lolote ujue mtu huyo hana zuri upande wake,na maneno mabaya au matusi dhidi yako inakuwa kama njia ya mkato ya kupunguza matatizo yake.Watu wa aina hii wanahitaji ushauri nasaha badala ya kuwatukana.Na kibaya zaidi ni kwamba ukimtukana chizi,basi watu watashindwa kutofautisha kati ya nani mzima au mwenye busara na nani chizi.

Lakini wapenda matusi hawa wananipa faraja moja kubwa.Kwamba hadi kufikia hatua ya kutukana kwa njia ya comment kwenye blogu hii inamaanisha walitumia muda wao kusoma nachoandika.Hiyo ni faraja kubwa kwangu kwani walengwa wangu wakuu ni watu makini na sio vichwa panzi kama hao mabingwa wa matusi.

Ujumbe wangu mfupi kwa wazembe hao wa kufikiri ni huu: kasheshe nilizokumbana nazo huko nyuma kutokana na mtizamo wangu ni mara alfu ya hivyo vijimatusi mnavyotuma kama comments.Kwahiyo endeleeni kupoteza muda wenu kutukana lakini mkae mkifahamu kuwa mnachofanya ni sawa na kutegemea damu kutoka kwenye jiwe.

Anyway,nasikitika kupoteza muda wangu muhimu kuwazungumzia wazushi hawa.Lakini yote katika yote,hivi ni vijimambo tu ambavyo once ukiingia kwenye fani ya kublogu lazima utakumbana navyo.

Bring it on!

2 comments:

  1. Tena hao ni wendawazimu maana wanategeme na kufikiri kwamba ufisadi utaendelea mille!!! La asha kila kitu kina mwisho wake na hasa suala haki mara nyingi inacheleshwa tu japokuwa lazima ipatikane. Bwana Chahali sishangai kwa hao wanakuandikia lugha chafu za kimaluhuni kwa sababu sifa ya mafisadi wote wote na hao watetezi wao ni wazuri sana kwenye divert topic. Na kuleta mada sisizokuwa na kichwa hata miguu. Angalia sasa umelazimika KUTUMIA muda, akili, hekima na utashi wako kuwajibu hawa wanyama(mafisadi na wapambe wao). Nikisema wanyama nina maana ya kuwa hawa mafisadi na wapambe wa wao kuwa wana akili tuu, na hiyo ni sifa ya mnyama pori ama wakufugwa. Binadamu hai na kamili anasifa hizi utashi, akili na hekima. HIvyo Bwana chahali husipoteze muda wako tena kuwajibu hawa wendawazimu

    ReplyDelete
  2. Asante sana bwana chahali ndo maana naona blog nyingi siku hizi huwa hawaweki comment sasa nimeelewa saabau.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube