21 Jul 2010

Kuna habari kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt Wilbrod Slaa,atakuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.Kwa mujibu wa gazeti la Daily News,Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana jana jijini Dar imemuomba Dkt Slaa kugombea nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo,Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto Kabwe,alinukuliwa akisema "Kamati Kuu (ya Chadema) imemuomba Dkt Slaa kuwa mgombea wa chama (katika nafasi ya urais)".Hata hivyo,Zitto alieleza kuwa uamuzi wa Kamati hiyo Kuu sio wa mwisho kwani itabidi mgombea urais wa chama hicho athibitishwe na Mkutano Mkuu wa chama hicho ambao umepangwa kufanyika Agosti 10.Kadhalika,Zitto hakuweza kueleza kama Dkt Slaa,ambaye gazeti hilo halikufanikiwa kumpata kuthibitisha habari hizo, amekubali ombi hilo au la.

Hata hivyo,vyanzo vya gazeti hilo katika kikao hicho (kilichokuwa kinaendelea wakati gazeti hilo linaenda mtamboni) vinaeleza kuwa Dkt Slaa,ambaye licha ya Ukatibu Mkuu wa Chadema ni Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya chama hicho, amekubali ombi hilo.Habari hiyo ya Dkt Slaa kukubali ombi la kugombea urais kwa tiketi ya Chadema imeandikwa pia kwenye mtandao maarufu kwa habari na mijadala makini,Jamii Forums.

Dokta Slaa amejikusanyia umaarufu mkubwa miongoni mwa Watanzania kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi.Japo ni mapema kubashiri nafasi yake katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu,ni dhahiri kuwa iwapo atasimama kama mgombea wa Chadema anaweza kutoa upinzani mkubwa kwa mgombea wa CCM,Rais (wa sasa) Jakaya Kikwete hususan katika namna chama hicho tawala kilinavyoonekana kama kichaka na hifadhi ya ufisadi na mafisadi.


2 comments:

 1. Kwa ushujaa na ujasiri alionesha katika kipindi chote huko nyuma na kuleta mwamko katika bunge hili letu lenye sifa kuwa na baadhi wabunge tangu mwanzo vikao vya bunge mpaka kuvunjwa kwa bunge bila kuuliza ama kuchangia jambo lolote, na pamoja kuwa matatizo lukuki yanayoikabili serikali na watendaji wake na pia wananchi na umaskini na ufakara wa kutupwa.

  Naamini Dk Slaa ni chaguo sahihi kwa kiti cha Urais kwa Tanzania ya sasa ili kuwa na serikali thabiti inatakiwa kuwa na kiongozi jasiri kupambana na uhozo uliopo serikalini na kwa maisha ya mtanzania kwa ujumla. Hivyo uwezo na ujasiri alionesha Dr Slaa naona ni chagua sahihi kabisa kwa sababu ana sifa zinazostahili na uwezo kulinganisha na mgombea wa CCM.

  Tanzania hii ya sasa inahitaji kiongozi anayeweza kutambua matatizo, kutafuta suluhisho na muda mfupi na mkakati muda mrefu na endelevu na kufanya tathmini ya kuendeleza miradi iliyopo na kuendelea kutambua matatizo yanayojitokeza.

  JK uwezo alionesha kutambua matatizo na siyo kupata suluhisho ya matatizo na kufanya tathmini endelevu. Hivyo Tanzania ya leo haihitaji Rais wa namna yake.

  Isipokuwa Chadema wanatakiwa kuwa makini na watu wanaojitokeza kusema wako tayari kumsaidia Dk Slaa katika kukampeni, kama hao waliokwisha shiriki kikamilifu katika kuhua nguvu na vuguvugu la kweli la vyama Tanzania...

  Kifupi watu kama Hao wakina Marando ni maadui wa siasa vyama vingi katika Tanzania yetu ya leo na ushahidi hupo na kila mtanzania mpenda demokrasia ya vyama vingi anafahamu fika kuhusu hili.

  Ningependa kusema na kuwakumbusha Chadema wanatakiwa kufikiria mara mbili kukaribisha watu wa namna ya kina Marando hasa kipindi hiki..

  ReplyDelete
 2. KWELI UMENENA JAMBO MARANDO HAFAI KUJIUNGA CHADEMA HUYO NI USALAMA WA TAIFA ASIJE AKATUHARIBIA HUYO

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.