27 Aug 2010

Inaelezwa kuwa vita vya mtandao (cyber war) ni tishio kubwa kwa Marekani kama ilivyo ugaidi.Na katika kujipanga vema kupambana na maadui wa nchi hiyo wanauweza kutumia mtandao kufanya mashambuli,Makao Makuu ya "Wizara" ya Ulinzi,Pentagon,imeanzisha mkakati wa kuajiri vijana wadogo wenye kipaji cha hali ya juu katika kuhujumu mtandao na kuufanya utekeleze matakwa ya mhujumu husika (hacking).


Katika kufanikisha zoezi hilo la kupata makuruta mwafaka,Pentagon ilisimamia shindano la uhujumu huo wa mtandao ambapo hackers vijana kadhaa walishiriki.Kichekesho ni kwamba katika kuonyesha uhodari wake katika fani hiyo,mmoj wa hackers hao alifanikiwa kuhujumu alama alizopewa na wasimamizi wa shindano hilo kabla matokeo hayajatangazwa.

Habari hii imenikumbusha kauli ya mwalimu wangu mmoja pale Mlimani,Profesa Ngware,aliyetupa "ukweli mchungu" kwamba "hivi kama wakati watoto wenu wanachezea vifuu ilhali wanangu wanacheza na kompyuta,mnatarajia watapokuwa wakubwa watakuwa na uwezo sawa wa akili?"


1 comment:

  1. HUU NIZAIDI YA UGAIDI WA KUJILIPUA! WACHA WATENGENEZE MAGAIDI WENGINE WATAKAO WASUMBUA WENYEWE HAPO BAADAYE MAANA INA SEMEKANA HATA OSAMA BIN LADEN WALIMTENGENEZA WENYEWE NA AKAWAGEUKA BAADAYE! HUYO KIJANA ALIYE HACK MTANDAO WAO WA MASHINDANO NI MOJA YA VIASHIRIA VYA UWEZEKANO WA KUGEUKWA BAADAYE.

    UMENIKUMBUSHA MBALI KWA KUREJEA USEMI WA PROF: SULEIMAN NGWARE WA UDSM

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube