15 Sept 2010

Dharau inayoonyeshwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kuendelea kutoa ahadi zaidi ilhali nyingi ya alizotoa mwaka 2005 hazijatimizwa,sasa imehamia kwa mkewe.Katika ukurasa wake wa Twitter (@salmakikwete),mke huyo wa Rais ameandika "“Tuwasikilize,tupembue chuya zikae upande wake,chenga upande wake na mchele ukae upande wake,tuseme lililo lililo la kweli,kama serikali haitatoza kodi,itaendeshaje shughuli zake?” Kauli hiyo pia inapatikana kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwanza,pamoja na kumheshimu kama First Lady lakini ilipaswa huyu mama akae kimya.Anatumia raslimali za taifa kumkapeni mumewe wakati anafahamu fika yeye (Salma) si mgombea.Huu ujasiri wa kinafiki wa kutetea kodi sijui unatoka wapi kwa vile tatizo letu kama taifa sio tu kwenye uzembe katika ukusanyaji kodi bali pia matumizi mabaya ya hata hiyo kodi ndogo inayokusanywa baada marafiki wa watawala kupewa misamaha ya kido kifisadi.

Hivi huyu mama anafahamu kuwa mumewe alipofanya ziara ya ghafla Bandari ya Dar es Salaam alitamka waziwazi kuwa anawafahamu watu wanaofanya ufisadi bandarini hapo?Na miongoni mwa ufisadi mkubwa sehemu hiyo ni dili za kukwepa kodi.

Sasa kama kweli ana uchungu na mapato ya serikali kwanini asimkumbushe mumewe kuhusu majina ya mafisadi wa Bandari ambao hadi dakika hii hajawataja au kuwasilisha majina yao kwa wahusika?

Kama unadhani namsingizi Kikwete hebu soma habari ifuatayoiliyochapishwa na gazeti la Nipashe la Machi 3 mwaka huu

Nawajua wanaosaidia kukwepa kodi TRA- Kikwete
2009-03-03 10:59:53
Na Joseph Mwendapole
Rais Jakaya Kikwete amesema ana orodha ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wasio waaminifu ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Alisema anaifanyia kazi orodha hiyo na akishamalizana nayo atamkabidhi Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, ili achunguze na kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaothibitika kujihusisha na vitendo hivyo.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na wadau wa bandari Tanzania alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni ufuatiliaji wa agizo alilotoa mwezi uliopita kupunguza msongamano wa makontena.
Alisema serikali haiwezi kuvumilia watu wanaoikosesha mapato.
Akitoa mfano namna wizi huo unavyofanywa, Rais Kikwete alisema wanaweza kuendesha zoezi hilo kwa simu ambapo mtu aliyeko Dubai anapewa maelezo namna atakavyojaza fomu ili mzigo wake usipite kwenye scanner, hali inayoweza kupitisha mizigo haramu kama dawa za kulevya.
Alisema wafanyakazi na wafanyabiashara hao wanatumia udanganyifu kuwa kontena hizo zimebeba mitumba, kumbe ndani ya mitumba hiyo wakati mwingine inatumika kufunika magari.
``Ninayo orodha ndefu na nitaikabidhi kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kitilya ili awafuatilie na ahakikishe anawatimua kazi mara moja wale watakaobainika wanahusika na mchezo huo ili tuanze upya,`` alisema.
Alisema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na wafanyakazi wanaokula njama za kuipotezea mapato.
Kikwete alisema bandarini kuna uzembe mkubwa ambao hauvumiliki na aliuagiza uongozi kuondoa matatizo yaliyopo badala ya kukaa na kunung`unika.
Alisema msongamano wa makontena umekuwa ukiisababishia serikali kukosa mapato mengi na alisisitiza kuwa bandari ni sehemu muhimu ambayo serikali haiwezi kuiacha iwe ya hovyo.
Akiwa katika kitengo cha kuchunguza bidhaa katika kontena, Tiscan, Rais Kikwete alisema maelezo aliyopewa na TPA yanatofautiana na yale aliyopewa na viongozi wa Tiscan.
``Hapa mbona mimi sielewi naomba mnieleweshe, hawa Tiscan wanasema wana uwezo wa kuchunguza hata makontena 200 kwa siku ila wanasema tatizo ni nyinyi hamleti kontena za kutosha... Jamani fanyeni kazi na muachane na visingizio na malalamiko,`` alisema Kikwete.
Aliagiza mamlaka hiyo impe taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa upunguzaji wa makontena ndani ya wiki mbili zijazo na aliahidi kutembelea tena bandari hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Forodha, Otieno Igogo, alimweleza Rais Kikwete kuwa wadau wa Bandari ya Dar es Salaam walikubaliana kulipa dola 30 ikiwa ni gharama za kuhamishia kontena moja katika bandari kavu.
Igogo alimweleza Rais kuwa ingawa wadau wote wamekuwa wakichangia, Kampuni ya Kimataifa ya Kupakua Kontena Bandarini (TICTS), imegoma kutoa fedha hizo.
Alisema dola 30 ambazo TICTS walipaswa kulipa kwa kila kontena linalohamishiwa bandari kavu kama wanavyolipa wadau wengine, zimekuwa zikitolewa na TPA.
Baada ya kauli hiyo ya Igogo, Rais alisema anashangaa kuona jeuri hiyo ya TICTS na kusema kuwa TPA ina mamlaka, lakini haitaki kuyatumia.
Kikwete alisema TPA imefanya vizuri kulipa gharama ambazo TICTS imekataa kuzilipa, lakini aliagiza mamlaka hiyo ihakikishe TICTS inazirudisha mara moja.
``Nyinyi mnashangaza sana, mna mamlaka, lakini hamyatumii... Sasa hizi gharama lazima walipe na wakiwashinda mwelezeni waziri na waziri akishindwa niambieni mimi,`` alisema.
Wakati huo huo, Kikwete alikataa maelezo marefu ambayo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraem Mgawe, alitaka kuyasoma mbele yake na badala yake akamtaka amweleze sababu za msongamano kutoma lizika.
Baada ya kuelezwa hivyo, Mgawe alimweleza Rais Kikwete kuwa kikosi kazi kilichoundwa kufuatia agizo lake kinaendelea kujitahidi kuondoa msongamano uliopo.
Alisema Mamlaka inatarajia kuwa utekelezaji wa mikakati iliyowekwa itafanikisha kupunguza hali ya msongamano mwezi Machi mwaka huu.
Mgawe alisema katika kipindi cha mwaka 2007/08, TPA ilihudumia tani milioni 6.239, ambalo ni ongezeko la tani 227,222 au asilimia 3.8 ikilinganishwa na tani milioni 6.003 zilizohudumiwa mwaka 2006/07.
Alisema katika kipindi hicho mamlaka ilipata ziada ya Sh. bilioni 37.879 kutokana na mapato ya Sh. bilioni 168.789 na matumizi ya Sh. bilioni 133.909.
SOURCE: NIPASHE

Wito wangu kwa Salma Kikwete ni simple: kama alikuwa anataka kugombea uongozi angegombea lakini sio kuendelea kutumia raslimali za taifa kumkampenia mumewe.Anapaswa kutambua kuwa raslimali hizo zinagharamiwa na walipa kodi ambapo wengi wao si wana-CCM (takwimu za karibuni zinaonyesha wanachama wa CCM ni takriban milioni 5 tu kati ya Watanzania takriban milioni 45).

Tunatambua kuwa Salma anataka kuendelea kuwa First Lady lakini asifanye hivyo kwa kuwabebesha gharama Watanzania wote hata wasio wana-CCM.Anaweza kuitumia WAMA kumfanyia kampeni mumewe lakini Watanzania hawataki kuona ufisadi wa mchana mweupe unaofanywa kwa misingi ya kifamilia.

Naamini mwanamama huyu anafuatilia habari za kimataifa,na hivyo amesikia yaliyomkumba Vera Chiluba,mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Zambia,Frederick Chiluba,aliyehukumiwa kwenda jela kwa ufisadi.

Ni vema Salma akasoma alama za nyakati ili pindi mumewe atakapokabidhi madaraka kwa Dokta Wilbroad Slaa hapo Novemba familia ya Kikwete isianze "kutafutana".

Na hiyo "tweet" yake ya kuchambua pumba na mchele nadhani ni vema akiielekeza kwa mumewe ambaye so far anaonekana kunogewa na "ugonjwa" wa kutoa ahadi.Mara uwanja wa ndege Kigoma,mara kuboresha kilimo cha kakao,mara atawapatia akinamama chanjo ya cervical cancer,mara vijiji 11 vya Mkinga vitapatiwa maji,mara hili mara lile alimradi ni "vurugu mechi ya ahadi".Kwani Rais wa Tanzania 2005-hadi sasa alikuwa nani kama sio Jakaya Mrisho Kikwete?Kwanini hayo anayoahidi sasa hakuyatekeleza katika awamu yake ya sasa?Na kwani tuamini kuwa atayatekeleza katika awamu yake ya mwisho-kipindi atakachokuwa bize kujitengenezea mazingira ya "kumpumzika kwa amani" kama Mkapa?

Blogu hii inawakumbusha tena wapiga kura kwamba Kikwete hayuko serious ndio maana ameamua kurejea nyingi ya ahadi zake za 2005 bila aibu wala kuwaomba msamaha Watanzania kwa kutozitekeleza.Kumrejesha tena Ikulu itakuwa ni kosa kubwa kupita kiasi kwani katika awamu yake ya mwisho atairejesha nchi yetu kwenye zama za mawe.

TANZANIA BILA UFISADI INAWEZEKANA
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA
TANZANIA BILA KIKWETE,SIO TU INAWEZEKANA,BALI NI MUHIMU LAZIMA KWA USTAWI WA TAIFA LETU.
CHAGUA DOKTA SLAA KWA UKOMBOZI NA "UHURU WA PILI",CHAGUA CHADEMA KWA TANZANIA YENYE NEEMA.


2 comments:

  1. kaka umesema yote...jana gari nilokuwa nasafiria kutoka Musoma lilisimamishwa Bunda mjini ati kusubiri msafara wa mama Mkubwa!

    Ukitazama magari yalokuwa kwenye msafara 99.5% yalikuwa ya serikali kutoka ile idara ya usalama yakiwa yamevikwa bendera za kijani kuwadanganya wasojua mambo!

    Polisi walikuwa wametanda barabara nim toka bunda hadi musoma huku patrol ikipita kama vile anakuja Bush!!!

    Bwana mkubwa amesema 'ahadi za elimu bure kwa wananchi wetu zinazotolewa ni uwongo...mbona zake alotoa 2005 pia ni bure? Anashindwa kujua kuwa kila ahadi inayotoelwa inatekelezeka...haoni ufisadi wa serikali yake na kikundi kinachomzunguka...'.

    Tunaibiwa mchana kweupeee!! Muda umefika wa kufanya maamuzi ya busara.

    ReplyDelete
  2. Mwl. Nyerere wala hakukosea alipomkataa KIKWETE asigombee nafasi ya raisi kwani alijua. Hana sifa za uongozi, anatumia madaraka yake vibaya...kwanini raisi yupo nje kila mara? anasafiri kwenda huku na huko kwani mabalozi wapo kwa ajili gani? Nadhani wanamwakilisha yeye..laini yeye nadhani aliweka nadhiri kuwa nikiwa raisi nitatembea dunia nzima kutanua wakati watu wengine wanaishi maisha ya tabu. Na hawana msaada wowote. Insikitisha sana kuona Mkewe naye anatumia pesa za serikali kumkampeinia mumewe.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.