20 Sept 2010

Blogu Hii inapenda kuungana na mwanahabari mkongwe,John Bwire, wa jarida la Raia Mwema,katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa baba yake mzazi .

Nimepata taarifa hizo kutoka kwa barua pepe aliyonitumia Bwire leo.

Kifo ni kifo,lakini kifo cha mzazi kinagusa mno.Hakuna maneno yanayoweza kuwa mwafaka kabisa kumliwaza mfiwa.Hata hivyo,kuna kauli ya kiroho inayoweza kuleta faraja na matumaini,kwamba SIE TULIMPENDA SANA MAREHEMU LAKINI BWANA MUNGU ALIMPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AMEAMUA KUMCHUKUA.Ni maneno yanayoweza kuonekana mepesi lakini yana uzito mkubwa.

Pumziko la milele Umpe ee Bwana,na Mwanga wa Milele Umwangazie,Astarehe kwa Amani

Amen

2 comments:

  1. Pole sana Bwana John Bwire! R.I.P mpendwa marehemu!

    ReplyDelete
  2. Inna Lillahi wainna ilaihi Raajiooun...(IWR) Bwire tupo pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na baba mzazi.RABBI Akupe nguvu umuombee maghufira kaburini na akhera...

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube