Showing posts with label TAARIFA ZA MSIBA. Show all posts
Showing posts with label TAARIFA ZA MSIBA. Show all posts

23 Jul 2011


Tunasikitika kuwatangazia kifo cha
Machira  NYITAMBE

Kilichotokea mchana leo huko  MUSOMA-TANZANIA

Mazishi yatafanyika huko Kirongwe, Shirati, katika mkoa wa Mara.


Marehemu ni baba mzazi wa:

Mrs Veronica Dibogo Nyitambe
Mrs Beatrice Nyitambe(Baba Mdogo)
Mr Soni Nyitambe (Baba Mdogo) ,


ambao wote wapo hapa Uingereza.

Msiba upo
14 Rothwell Walk
Caversham
Reading

RG4 5DB

Kwa mawasiliano zaidi tumia simu zifuatazo:
Bernard Chisumo
Mob: (0) 787 612 6862
Home: (0) 118 954 5890 
---------------------------------------------------------------- 

POLENI SANA WAFIWA.SIE TULIMPENDA MAREHEMU LAKINI BWANA ALIMPENDA ZAIDI

23 Jun 2011


 
Ndugu, Jamaa, na Marafiki, Watanzania wote;
Kwa masikitiko makubwa tunawataarifu ya kwamba, tumepokea habari za msiba wa mwenzetu EDGAR KILEKE (KAKA DICK). Msiba umetokea leo huko Leicester Uingereza. Marehemu Edgar amefariki baada ya kuugua cancer ya Ini. 

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kueleke anyumbani kwa mazishi inafanyika. Tunawaomba wote, kwa moyo wa upendo na utoaji, tusaidiane ili tukamilishe maandalizi haya na mwenzetu ili aweze kwenda kupumzishwa kwenye makao yake ya milele huko nyumbani Tanzania. Tunatanguliza shukurani za dhati kwa michango yenu. Wanaoweza kuwatembelea wafiwa na kutoa pole mnakaribishwa na msiba upo kwenye address hapo chini:

89 Stevenson Drive
LE3 9AD
Leicester

Kwa maelezo ya ziada wasiliana na;
Asaa Ali  07951644936
au

Fauzia Musa 07943962628

Kama hutaweza kufika Leicester, unaweza kutuma mchango wako kwa:
A A KAKOZI
Account Number 85065992
Sort Code: 09-01-27
Bank: Santander


Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.


Asanteni.


R.I.P EDGAR!!


Imetumwa na Miss Jestina

20 Sept 2010

Blogu Hii inapenda kuungana na mwanahabari mkongwe,John Bwire, wa jarida la Raia Mwema,katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa baba yake mzazi .

Nimepata taarifa hizo kutoka kwa barua pepe aliyonitumia Bwire leo.

Kifo ni kifo,lakini kifo cha mzazi kinagusa mno.Hakuna maneno yanayoweza kuwa mwafaka kabisa kumliwaza mfiwa.Hata hivyo,kuna kauli ya kiroho inayoweza kuleta faraja na matumaini,kwamba SIE TULIMPENDA SANA MAREHEMU LAKINI BWANA MUNGU ALIMPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AMEAMUA KUMCHUKUA.Ni maneno yanayoweza kuonekana mepesi lakini yana uzito mkubwa.

Pumziko la milele Umpe ee Bwana,na Mwanga wa Milele Umwangazie,Astarehe kwa Amani

Amen

18 Sept 2010


Tunasikitiza kutangaza kifo cha Pr. Joseph Shem Onyango (pichani akiwa na mkewe na wajukuu) Kilichotokea jana mchana Kihonda, Morogoro kutokana na ajali ya barabarani. Mchungaji alikuwa akielekea kwenye kituo cha basi tayari kwa safari ya kwenda dar kushiriki katika sabato ya wageni jumamosi tarehe 18.9.10 kwenye kanisa la Tegeta. Marehemu alizaliwa 1936 na amekuwa akililitumika kanisa la waadeventista wasabato kwa zaidi ya miaka 40, Pr. atakumbukwa sana na watu wengi africa mashariki kutokana na huduma zake kwenye kanisa za kaya na familia pamoja na sera za ndoa.

Mazishi yanategemewa kufanyika alhamisi mji wa morogoro.

Asanteni

Frank Eyembe
Urban Pulse Creative

BLOGU HII INATOA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA.BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE

23 Jun 2009

Pichani,Mwanasoshojia akimuaga Mzaa chema.

BLOGU HII INATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA KIFO CHA MAMA MZAZI WA BLOGA MWANASOSHOLOJIA.HAKUNA MANENO MWAFAKA YANAYOWEZA KUKULIWAZA WEWE BINAFSI NA FAMILIA YENU KWA UJUMLA,LAKINI TUAMINI KUWA MUNGU AMEMPENDA MAREHEMU ZAIDI YETU,NA NDIO MAANA AMEMCHUKUA.NA KWA VILE MUNGU NI WA UPENDO,BASI TUNA HAKIKA ATAMPATIA MAREHEMU PUMZIKO LA AMANI NA RAHA YA MILELE.

POLE SANA,MWANASOSHOLOJIA.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.