26 Oct 2010


Nimetumiwa barua pepe yenye habari ifuatayo nami naiwasilisha kama ilivyo


Taarifa kutoka Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia mkoani Mbeya zinasema kuwa lori la kampuni ya Azam linalomilikiwa na mfanyabiasha maarufu Bakhresa leo hii tarehe 18 Oktoba, 2010, limekamatwa likiwa na shehena kubwa la karatasi za kupigia kura zitakazotumika uchaguzi mkuu Oktoba 31.
Maafisa wa TRA tunduma walishtuka baada ya kukuta karatasi hizo za kupigia kura zimefichwa kwenye shehena ya vipodozi. Inasemekana kuwa mzigo huo wa karatasi za kupiga kura ulitokea Afrika Kusini na ulipakiwa kwenye gari la Azam kutoka kwenye gari lililotoka na mzigo kutoka Afrika Kusini.
Taarifa zinasema kuwa lori hilo linashikiliwa na TRA na mzigo huo umekuwa sealed. Kuna hofu kuwa vigogo wenye njama za kuiba kura wanaweza kujaribu kufuta ushahidi kuhusu kukamatwa kwa karatasi hizi za kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, karatasi hizo za kupiga kura tayari zimewekewa tiki kumchagua Jakaya Kikwete wa CCM na lengo ni kuwa zisambazwe kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini na zihesabiwe kama kura halali.
Tafadhali mwenye taarifa zaidi kutoka mpakani Tunduma atupatie ukweli wa jambo hili
" ........ Wadau huu ni ukweli mtupu magari mawili ya A.A.Bahresa (named Azam on board)T 501AEM na T 263 AJN yako hapa kituo kikuu cha polisi mkoa Mbeya,binafsi nimeona hizo karatasi za kura ambazo JK kapigiwa kura ya ndio na ziko kama karatasi milioni tano kwa haraka haraka hope police watatoa taarifa kamili,wametutoa nje sijui wanazichakachua "

Nawasilisha kwa taarifa na ushahidi

4 comments:

 1. WAZUSHI...Mmeanza sasa ati karatasi za kura zimekamatwa na mdau ati ameziona takriban milioni tano...UPUUZI NA HATUDANGANYIKI...
  Acha nikudokeze...taratibu za uopigaji kura ni kuwa watakuwepo mawakala wa vyama vyote kikiwamo chama cha masia wenu.na masanduku yale ni transparent unaona mpaka ndani...na kila kituo kuna orodha ya wapiga kura..na shahada ya kura ina serial namba ambazo zitaorodheshwa pembeni mwa jina lako kabla hujakabidhiwa kuingia sehemu ya siri kupiga kura.Sas huo upuuzi unaoandika kwa wino mwekundu ati shahada zimekamatwa kutoka Afrika kusini na ati malori ya Bakhresa yamekamatwa nazo...unataka tuamini upuuzi huo???Waangalizi wa kitaifa na kimataifa watakuwepo vituoni mpaka zoezi la kuhesabu kura litakapokamilika..hizo shahada feki utaziweka wewe na wapuuzi wenzako kwa njia ya maruhani????

  ReplyDelete
 2. ukweli unauma

  ReplyDelete
 3. waangalizi wa kimataifa hadi namtumbo? huko hao mawakala hamna ni wenyeviti tu wa ccm,barua zimekamatwa mwanza jinsi ya kuiba kura kwa vijana, vyuo havijafunguliwa ili wanavyuo wasipige kura,unamdanganya nani

  ReplyDelete
 4. Nilitegema umeanza kupona Kichaa chako Laiza kumbe bado unaumwa rudi wodini ya vichaa haraka kabla mambo hajakuaribikia tena kama hapo siku za nyuma

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube