26 Oct 2010

Add caption


WAINGEREZA WANA MSEMO "IF SOMEONE HAS SOMETHING BAD TO SAY ABOUT YOU,IT'S PROBABLY BECAUSE THEY HAVE DON'T HAVE NOTHING GOOD TO SAY ABOUT THEMSELVES",YAANI KWA KISWAHILI,UKIONA MTU ANA BAYA LA KUSEMA KUHUSU WEWE BASI PENGINE NI KWA VILE HANA JEMA LA KUSEMA KUHUSU YEYE MWENYEWE.

RAIS ALIYE MADARAKANI NI JAKAYA MRISHO KIKWETE.CHAMA KILICHO MADARAKANI NI CHAMA CHA MAPINDUZI.SASA CHA KUSHANGAZA,AJENDA KUBWA YA KIKWETE NA CCM IMEKUWA KUHUSU "KWANINI DAKTA SLAA HAFAI,KWANINI CHADEMA WAONGO,KWANINI AHADI ZA DKT SLAA/CHADEMA HAZITEKELEZEKI" NA UPUUZI MWINGINE KAMA HUO.HIVI RAIS ALIYEKUWA MADARAKANI MIAKA MITANO NA ANAYETOKA CHAMA AMBALO LIMETUTAWALA MIAKA NENDA MIAKA RUDI HAWANA LA KUTUELEZA KUHUSU WAO WENYEWE BALI KUMVALIA NJUGA DOKTA SLAA NA CHADEMA KANA KWAMBA AKINA LIPUMBA NA WAGOMBEA URAIS WENGINE WANAGOMBEA UBUNGE AU UDIWANI?

JIBU LIPO KWENYE HUO MSEMO WA WAINGEREZA.KIKWETE NA CCM HAWANA JIPYA AU ZURI LA KUWAELEZA WATANZANIA ZAIDI YA KUDURUFU AHADI ZA MWAKA 1995,2000 NA ZAIDI 2005.HAWANA JIPYA ZAIDI YA KUBAHATISHA MBINU YAO MAARUFU YA "TUPENI KURA TUMALIZIE TULIYOANZA AWAMU HII".YAANI TUWAPE TENA KURA WAMALIZIE KUMALIZA RASLIMALI ZA TAIFA? HELL NO!TUWAPE TENA MIAKA MITANO WAMALIZIE UBIA WAO NA MAFISADI KUSAFISHA KILA KILICHOPO.HAPANA,NO,NEVER!

WAMETUNYANYASA KIASI CHA KUTOSHA.
WAMETUDHARAU KIASI CHA KUTOSHA (NDIO MANA AHADI LEO HAWATAKI KUOMBA MSAMAHA KWA MAKOSA YA UFISADI)
WAMETUTESA KIASI CHA KUTOSHA.
UMEFIKA WAKATI WA KUWAAMBIA NOT ANY MORE. IMETOSHA.WAMETUIBIA VYA KUTOSHA LAKINI SASA TUKIWAREJESHA TENA MADARAKANI SIO TU WATATUFILISI BALI PIA TUTAONEKANA WAJINGA KWA KUWARUHUSU WATUFANYE WAJINGA.

CHAGUA DOKTA WILBROAD SLAA KWA TANZANIA MPYA YENYE NEEMA NA MAENDELEO
MSTAAFISHE KIKWETE KWA MANUFAA YA UMMA
WATIMUE MAFISADI TUREJESHE NCHI MIKONONI MWETU

INAWEZEKANA.TIMIZA WAJIBU WAKO KWA KUMPIGIA KURA DOKTA SLAA HAPO JUMAPILI1 comment:

  1. Na ajenda kubwa ya kwako ni kwa nini JK hafai..kwa nini CCM haifai...inafaa Chadema anafaa Dk Slaa...Jana nilisikiliza live hotuba za Marando na Slaa pale mwembe yanga...wao wote walizungumza na kudai kikwete hafai ati Dk Slaa ndio jibu la watu.....ati msafara wake jumapili uliongozwa na wananchi na magari yakampisha kwa heshima....aaah...anasahau watanzania walivyo wakiwa barabarani kwa shughuli yoyote ile....labda hana kumbukumbu ya yaliyojiri mwembechai pale Sheikh ponda alipokuwa anasakwa na wananchi wakaanzisha mradi wa kuvamia magari....Kumpisha kwa magari ni kuogopa magari yasiharibiwe na mafedhuli..au vibaka..Haya naye Mabere Nyaucho akatoa uongo wa mwaka...ati mwaka 1995 Mwalimu alimkataa mgombea wa CCM hadharani kule Musoma na kudai ati mwizi anastahili kuwa gerezani...lakini ajabu ni kwamba mgombea wa CCM ndiye aliyeshinda ubunge wakati huo...jamani hizi mnazopiga ni kelele za mlango tu...hazitunyimi usingizi..msema kweli ni oktoba 31....twendeni wote...wewe kampe Slaa nami nampa JK halafu tuhesabu mdai tumechakachua

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.