28 Nov 2010


Waislam wakiwa kwenye swala.Picha hii haihusiani moja kwa moja na habari ifuatayo
Waislam wenye msimamo mkali wanashukiwa kuyachoma moto majengo mawili ya kanisa huko Zanzibar,tukio lililotokea Jumapili iliyopita huku waumini wa makanisa hayo wakipokea vitisho vya kuuawa.

Majengo hayo ya Kanisa la Assemblies of God (TAG) na Evangelical Assemblies of God Zanzibar (EAGZ) katika kijiji cha Masingini kilichopo kilomita 5 kutoka mjini-kati Zanzibar yalichomwa moto takriban saa 2 usiku,kwa mujibu wa Askofu Fabien Obeid wa EAGZ.Polisi wa Mwera walipata taarifa ya tukio hilo kesho yake asubuhi.

Matukio hayo ni mwendelezo wa vitendo vya kuwatisha Wakristo katika eneo hilo lenye Waislam wengi,na kuibua hofu kwamba Waislam wenye msimamo mkali wanaweza kudiriki kufanya lolote lile kuzuwia ustawi wa Ukristo.

“Muislam mmoja alisikika akisema, ‘Tumesafisha eneo letu kwa kuharibu makanisa mawili,na sasa tuna mpango wa kuwaua waumini wa makanisa haya mawili-hatutaruhusu kanisa kujengwa tena,’” alisema muumini mmoja wa kanisa ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Jengo hilo la matofali la TAG lilikuwa katika hatua za mwisho za ujenzi,na kwa mara ya kwanza Jumapili hiyo waumini walifanya ibada katika jingo hilo jipya.Jengo la EAGZ ambalo waumini takrban 30 walihudhuria ibada lilikuwa la udongo.

Pasta Michael Maganga wa EAGZ na Pasta Dickson Kaganga wa TAG walieleza hofu yao kuhusu hatma ya kanisa hapo Masingini.Mapasta wa Zanzibar walitarajiwa kukutana jana (Jumamosi) kujadili namna ya kukabiliana na uharibifu huo,alieleza Mwenyekiti wa Usharika wa Mapasta Zanzibar,Askofu Lonard Masasa wa Kanisa la EAGT.

Kwa muda mrefu Waislam wenye msimamo mkali visiwani Zanzibar,wanaoungwa mkono na baadhi ya viongozi wa serikali katika maeneo husika,wamekwaza uwezekano wa Wakristo kupata ardhi kwa minajili ya ujenzi wa majengo ya ibada.Kuna nyakati ambapo wamebomoa majengo yaliyopo na badala yake kuanzisha ujenzi wa misikiti.

Huku wakikanganywa na kutopata ushirikiano wa serikali katika kuwashughulikia wahusika wa matukio hayo,viongozi wa makanisa wameeleza kuwa uwezekano wa waliochoma moto majengo hayo kukamatwa ni mdogo.Mara nyingi,serikali huegemea upande wa wanaofanya matukio hayo,kuchelewesdha uchunguzi kwa hofu ya kuwaudhi Waislam walio wengi ambao wanapinga kuenea kwa Ukristo.

Mwaka jana,maafisa wa serikali katika eneo la Mwanyanya-Mtoni waliungana na Waislam wa eneo hilo kujenga msikiti katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la EAGZ,alieleza Pasta Paulo Kamole Masegi.

Pata Masegi alinunua ardhi mwezi Aprili mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa katika eneo hilo la Mwanyanya-Mtoni,na kufikia mwezi Novemba mwaka huohuo tayari kulikuwa na jengo lililotumika kama sehemu ya ibada kwa muda.Muda si mrefu Waislam wa eneo hilo walipinga hatua hiyo.

Mwezi Agosti mwaka jana,Waislam hao walianza ujenzi wa msikiti futi tatu tu kutoka kitalu cha kanisa.Mwezi Novemba mwaka huohuo,Pasta Masegi alianza ujenzi wa kanisa la kudumu.Waislam wenye hasira walivamnia eneo hilo na kubomoa msingi wa jengo hilo,alieleza Pasta huyo.

Viongozi wa kanisa waliripoti tukio hilo kwa polisi,ambao hawakuchukua hatua yoyote- na walikataa kutoa ripoti ya tukio,hivyo kukwamisha suala hilo kufikishwa mahakamani,alisema Pasta Masegi.

Wakati huohuo,ujenzi wa msikiti ulikamilika mwezi Desemba (mwaka jana).Hatma ya mpango wa ujenzi wa kanisa ilielekea kufikia ukomo mapema mwaka huu baada ya Mkuu wa Wilaya Ali Mohammed Ali kumfahamisha Pasta Masegi kuwa hana haki ya kufanya ibada katika jengo husika.

Kihistoria, wafanyabiashara wa Kiislam kutoka Ghuba ya Uajemi walifika visiwani Zanzibar mapema karne ya 10 baada ya kusukumwa na pepo za monsoon katika Ghuba ya Aden.Muungano wa visiwa hivyo na Tanganyika mwaka 1964 (na kuunda Tanzania) uliwaacha Waislam visiwani humo wakiwa na hofu kuhusu Ukristo,wakiuona kama njia inayoweza kutumiwa na Tanzania Bara kuwatawala,na tangu wakati huo kumekuwa na hali ya mashaka.


14 comments:

 1. Chahali, mimi ni msomaji sana wa blog yako, but inaonekana unachukia sana uislam sababu una bold sana habari za waislam tena unachagua mbaya tu kila nisomapo blog yako b4 chaguzi ilikuwa ccm sasa umehamia kwa uislam, why? cha ajabu unazungumzia kuchomwa moto kanisa unatoa picha ya watu wanaswali!!tafuta basi na habari nzuri pia zipo nyingi tu kuhusu uislam

  ReplyDelete
 2. Mkuu,asante kwa comment.Kama nilivyoandika hapo chini ya picha,taswira hiyo haihusiani moja kwa moja na habari husika.Ni picha tu ya waumini wanaoswali.

  Nilitarajia badala ya kunilaumu kuwa nauchukia Uislamu ungewashutumu hao waliofanya vitendo vya kihalifu.

  Pia naomba kukuhakikishia kuwa japo mie ni Mkristo,sina chuki yoyote na Waislamu.Naamini licha ya tofauti zetu kidini,sote tunapaswa kukemea watu wanaogeuza dini kuwa chanzo cha migogoro.Wanaonifahamu wanaweza kukuthibitishia ukaribu wangu na Uislam na Waislam.Naomba uamini hivyo.

  ReplyDelete
 3. Waislamu ni balaa la dunia. Kuwachukia ni halali na haki. Hata Muhammad aliwachukia akawaachia mfumo laanifu na mchafu kuliko hata nguruwe.

  ReplyDelete
 4. Back again Chahali, mtu akisoma heading yako then akaangalia picha b4 hajasoma maelezo uliyoandika, atakuwa na tafsiri kama, kuswali inamaanisha msimamo mkali which implies matendo mabaya, as u know picture speaks more than words. I dont blame u coz is just mtazamo wako binafsi but jaribu kuweka picha zinazo relate na habari directly. Huyo Anonymous 29/11/2010 02.05.bahati mbaya amebarikiwa upungufu wa mawazo pia ufinyu wa elimu unachangia

  ReplyDelete
 5. Nimekuelewa ndugu yangu.Nitabadilisha hiyo picha.Samahani kama nimekwaza.

  ReplyDelete
 6. Hao ni kawaida yao, waislamu mnafundishwa kuwachukukia wakristo mkiwa bado watoto wadogo, hiyo ni imo katika imani zenu. Kama ingekuwa hivyo basi nyote si muende mukaishi huko uarabuni, mbona mkifika nchi za watu mnaruhusiwa kujenga misikiti yenu na kuswali, huko kwenu mnaona wenzenu hawana haki grow up guys. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu muchungu.Anonymous 29 he is right na hajapungukiwa na kitu chochote na elimu anayo tosha zaidi yako 29/11 04.20

  ReplyDelete
 7. nimechoka na watu kutumia dunia kama excuse ya kuact kama wanyama, hamna dini yeyote inafundisha kuchukia watu, kama dini inakufundisha chuki basi sio dini, sijui kwanini hatuwezi tukakaa kila mtu akaamini anavyotaka tueshimiane choice zetu, kuchoma kanisa unaprove nini, hata sielewi hata kidogo, kwanza waislam wa Kiafrica mnavojipendekeza kwa waarabu, they hate black people, sijui kupindekeza ndio nini, hasa hasa watawatumia kuwapandisha ndege, wake up and form your opinion ...

  ReplyDelete
 8. Ewe uliemtukana muhamad na waislam,allah akusamehe na akuongoze njia ya haki... Amen

  ReplyDelete
 9. vijana msikurupuke na udini someni upate kufuta ujinga mnafahamu zanzibar ukristo umefika kabla ya mama zenu ba babu zenu tena wanaishi kwa upendo somedi dini zenu YESSU NA MOHAMAD NI siyo wazungu ni watu wenye asili ya kiarabu mayahudi ni ndugu na warabu na asili yao ni siriya na lebanon siyo warabu wote waislam wapo arab jush jee unajuwa warabu na mayahudi ni kizazi kilichotoka kwa mtume Gink solomo ni babu wa wayahudi na wawarabu jee wewe mmatumbi unatokeya wapi? YESSU KAJA KWAAJILI YA KONDOO WALIOPOTEYA WA KIYAHUDI NA MOHAMAD KAJA KWA AJILI YA WARABU SASA WEWE MMATUMBI USIKURUPUKE

  ReplyDelete
 10. Kwa mtazamo wangu, wewe unachuki binafsi na waislamu, habari zako nyingi unavyo report unajaribu kutengeneza chuki katika jamii..Hii ni moja wapo..

  ReplyDelete
 11. Sasa bwana Chahali naona mwelekeo wa Blog na maoni yanaelekea njia isiyo sahihi, kujadili vitu vinanvyofundishwa kila iku makanisani na misikitini lakini havijaweza kuwabidilisha waumini kwenda huduma za waganga wa kienyeji

  ReplyDelete
 12. Sasa Anonymous hapo juu,yaani watu wakichoma majengo ya kanisa kisha ikaripotiwa (pasipo kuongeza mtazamo wangu binafsi) bado unashutumu kuwa nina chuki dhidi ya Waislam?Mbona wewe mwenye upendo umesbindwa japo kukemea uhalifu huo?Kumbuka dini ni upendo,iwe Uislam au Ukristo.Binafsi siwezi kuwahukumu Waislam wote kwa vile tu kikundi kidogo kimetenda uhalifu dhidi ya Wakristo,let alone kukuhukumu wewe.Katika imani yangu,tunafundishwa kujiepusha na kuwahukumu wengine lest be judged too.Mwenye mamlaka ya hukumu ni Muumba pekee.However,asante kwa maoni yako hata kama siafikiani nayo.

  ReplyDelete
 13. ilipochomwa Quran Hatukukusikia au ulikuwa huna habari hizo
  mlikaa kimya wewe na Rais wako mstafu Ali hasani na sasa
  atapata vibao viwili paaa paaaa

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.