6 Jan 2011


10 wauwawa kwenye ghasia mjini Arusha

Dr Wilbroad Slaa naye pia amekamatwa
Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.

Baadaye polisi pia walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Oktoba Dr Wilbroad Slaa.

Taarifa zinasema biashara kadhaa zilichomwa moto kwenye vurugu hizo.

Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.

Bwana Slaa amenukuliwa akisema maandamano hayo yalikuwa ya kupinga ufisadi katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete.

Polisi walifyatua risasi hewani mara kadhaa kutoa tahadhari kwa maelfu ya wafuasi waliokwenda kutaka viongozi wao waachiwe huru, na baadaye wakafyatua gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Walioshuhudia wanasema Polisi waliendelea kufyatua risasi mchana kutwa, huku wafuasi wa CHADEMA wakiendelea kukabiliana na askari Polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Arusha.

Kwenye mkutano huo wa kisiasa, Dr Slaa aliwataka Polisi kumwachilia huru Bwana Mbowe na wengine, na pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.

Hadi kufikia Jumatano jioni hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na serikali kuhusu mzozo huo.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Tanzania tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais ambao vyama vya upinzani vinadai ulikuwa na udanganyifu.

Kufuatia uchaguzi huo shinikizo zinaendelea za kutaka Tanzania iwe na katiba mpya tofauti na iliyopo sasa, ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani yanapotangazwa na tume ya uchaguzi.

CHANZO: BBC Swahili

3 comments:

  1. Jamani hivi kwenye CCM hamna mtu aliyebaki mwenye busara kidogo yakuokoa jahazi lisizame. Kikwete na Makamba, Rostam et al wameachiwa waendeshe chama kama family business. Mbona all these was unnecessary si wangemaliza mazungumzo kama walivyoahidi on Jan 05 au walifikiri wananchi wote ni wajinga. It is not about Chadema anymore it is about Tanzanian people. Kikwete you do not OWN THIS COUNTRY FOR HEAVEN SAKE??? Mbona inakua ngumu washauri wake au hao wazee wa CCM kumueleza hilo. Kuandamana kwa amani ni haki ya mtu sio lazima uruhusu wewe!! Kwani unachoogopa ni nini hasa kama hakuna kitu unachoficha?? kwani wakisema wewe ni fisadi kama wewe sio fisadi why do you worry??? Action zako na serikali yako zinadhihirisha kabisa kila Dr. Slaa analosema ni kweli haiwezekani u-react kama mtu ambaye ni guilty kama wewe sio guilty. Kumbuka wajanja kama Saadam Hussein, Mobutu, Moi etc wameishia kuwa hadithi tu, hakuna kisichowezekana my friend. Nanona muda wakubembelezana na hawa watu umekwisha no more soft talk ni action tu kwakwenda mbele. It is not over I assure you it is not over history will be made in Arusha soon or later.

    ReplyDelete
  2. Kiongozi kuwa na leadership skills ni muhimu sana sio watu wanajibambikizia tu uongozi.Makamba alimdhihaki Lowassa kuhusu kutatua mgogoro wa Arusha. Pamoja na madhaifu ya Lowassa, Lowassa ni mwenyeji wa Arusha na anaelewa fika strategy za kutatua mgogoro kwa watu wa eneo la pale ndio maana alisisitiza mazungumzo. Sasa mzee Makamba anataka kufanya staili za uswahilini za mipasho na kusutana hiyo Arusha haiwezi ku-work.The people there (wenyeji) use more actions than words. Watu wa Arusha huwezi ukawakandamiza wakanyamaza huo ni ukweli halisi. Just mark my words, watalipiza in one way or another. Hii haijaisha, nakumbuka migogoro ya kidini, nakumbuka migogoro wa watu wa machimboni(wana-apollo),nakumbuka migogoro ya ardhi etc unafikiri kitu kimeisha baada ya a month watu wanalipuka (lipa kisasi) na mgogoro unaanza upya. I think this is total failure in leadership. Nampongeza Luten Mstaafu Olle Molleiment kwakukemea viongozi wa CCM waziwazi kwamba wamelewa madaraka (Source- Mwananchi). Huwezi kuruhusu vyama vingi alafu ukawanyima uhuru wakujieleza au kukupa-challenge. It is impossible!JK na Makamba lazima muelewe mmeshindwa uongozi na mmezamisha jahazi. Kama kuna wana-CCM waliona mapenzi na chama they need to act quickly. JK had already failed as a president a while ago ndio maana akachukua nchi kwanguvu, sasa naona na huu uongozi wa chama umeshamshinda. I can smell something bad before 2015!

    ReplyDelete
  3. HATUONGOZWI NA MAJANGILI, WAUWAJI, WALAFI, WAKANDAMIZAJI, WABAKAJI, MAFISADI WAKUBWA! WASHAMWAGA DAMU YA WATANZANIA, WANAONGOZA VIPI NCHI? UTAMTAMBUAJE RAISI WAKO AKIWA ANA C.V ILIYOJAA DAMU! WANANCHI NDIO TUNA MAAMUZI, ATOKE HUYU JAMAA, NA WALA SI KUSUBIRI 2015

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.