14 Feb 2011


Leo ni Siku ya Mtakatifu Valentine,maarufu kama Siku ya Wapendanao,au Valentine's Day kwa kimombo. Pengine ni vema kuadhimisha siku hii kwa kutafakari umuhimu wa upendo.

Binafsi,si muumini mzuri wa siku zinazoambatana na matukio.Kwa mfano,mara nyingi huwa naadhimisha siku yangu ya kuzaliwa kwa sala na tafakuri ya miaka iliyopita na ijayo,Mungu akinijalia.Kwa wengine,siku ya kuzaliwa ni wakati wa kuingia gharama zisizo na umuhimu kwa sherehe kubwa zinazowaacha wakiwa na hali ngumu baadaye.Japo ni muhimu kufanya maadhimisho ya siku muhimu kama ya kuzaliwa lakini kuna umuhimu gani kama siku hiyo inabaki kuwa "siku muhimu" tu pasipo kuangalia wapi umetoka,ulipo na unakoelekea?

Na katika mantiki hiyohiyo,Siku ya Wapendanao inakuwa tu na umuhimu kama upendo utatafsiriwa kwa dhamira na vitendo.Kuna umuhimu gani wa kuadhimisha Siku ya Wapendanao kwa kadi za gharama na vinywaji ilhali umewasahau wanaohitaji upendo wako?

Wengi tunaelewa namna baadhi ya wenzetu wanavyoiogopa siku hii kutokana na kuwa na ma-Valentine wengi.Na miongoni mwa hawa ni wale wanaoadhimisha siku hii na "nyumba ndogo" huku wakiacha visingizio kwa wapenzi wao halisi.Hali hiyo inapoteza maana nzima ya siku hii.Haiwezekani mtu kudai anaadhimisha Siku ya Wapendanao kwa kumsaliti mpenzi wake.

Vinginevyo,nawatakia Siku njema ya Wapendanao nikiamini kuwa maadhimisho ya siku hii yatakuwa ya dhamira zaidi kuliko vitendo pekee.

1 comment:

  1. kaka uko sahihi kwa hii post,kwan watu wanatumia cku hii kuhararisha uzinzi na kuacha dhamira kuu ya cku hii.inapaswa tujiheshimu jaman kwan wanaohitaji upendo wako ni wengi ila wewe unatumia cku hii kufanya mambo amabayo hata mungu hayampendezi

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube