Showing posts with label VALENTINE'S DAY. Show all posts
Showing posts with label VALENTINE'S DAY. Show all posts

14 Feb 2013


Blogu hii inawatakia heri na baraka kwa siku hiimaalum kwa wapendano (Valentine's Day). Hapo juu nimedai Valentine wangu ni HUYU...Guess what? Si mtu bali ni social media. Siku kama leo, miaka mitano iliyopita (Februari 14, 2008) nilijiunga na mtandao wa kijamii wa TWITTER. Kwahiyo wakati wapendwa wasomaji wa blogu hii mnasherehekea Valentine's Day yenu, mie nina sherehe ya ziada: KUTIMIZA MIAKA MITANO KATIKA TWITTER.

Twitter imeniwezesha kufahamiana na watu wa kila aina, na hadi muda huu ninaposti makala hii nina followers 2,239.Natambua kuwa mie si mwepesi sana wa ku-follow back lakini ninaamini kila anayeni-follow atakubaliana nami kwamba hawaoni tofauti yoyote ya kuwa followed au kutokuwa followed nami kwani nipo interactive na kila mtu: SIBAGUI SICHAGUI. Na si kama ninajisifu lakini kwangu kila binti ninamu-address kama DADANGU na kwa wanaume wenzangu ninapenda kuwa-address kaka MKUU.

Kama nilivyobainisha hapo awali, Twitter imeniwezesha kufahamiana na watu wa kada mbalimbali, kutoka bankers wa kimataifa kama @chiume hadi wasanii kama @MwanaFA, kutoka Waheshimiwa kama @JMakamba hadi viongozi wa makampuni makubwa ya kimataifa kama @Makambas, na kutoka wanaharakati kama @YerickoNyerere na @MariaSTsehai hadi supamodo kama @FlavianaMatata na @Mariadkinawa , kutoka kwa wazalendo kama @dgtlUbun2 hadi wanasiasa kama @nape_nnauye na @shyrosebhanji, na kutoka kwa marafiki waliopo kama @kundaelyjr na @nanyaro_ na 'lost friends' kama @annieTanzania hadi wajasiriamali kama @AfricanGenesis na @IddaKabendera bila kumsahau 'rafiki mrembo' @bootyferrari360 na  mdogo wangu wa dhati @iMalaika....orodha ni ndefu,na kama sikukutaja haimaanishi kuwa huna umuhimu kwangu.

WAKATI NINAADHIMISHA MIAKA MITANO TANGU NIJIUNGE NA TWITTER NAOMBA KUWATAKIA VALENTINE'S DAY NJEMA KWENU NYOTE. TUENDELEE KUPENDANA

14 Feb 2012

14 Feb 2011


Leo ni Siku ya Mtakatifu Valentine,maarufu kama Siku ya Wapendanao,au Valentine's Day kwa kimombo. Pengine ni vema kuadhimisha siku hii kwa kutafakari umuhimu wa upendo.

Binafsi,si muumini mzuri wa siku zinazoambatana na matukio.Kwa mfano,mara nyingi huwa naadhimisha siku yangu ya kuzaliwa kwa sala na tafakuri ya miaka iliyopita na ijayo,Mungu akinijalia.Kwa wengine,siku ya kuzaliwa ni wakati wa kuingia gharama zisizo na umuhimu kwa sherehe kubwa zinazowaacha wakiwa na hali ngumu baadaye.Japo ni muhimu kufanya maadhimisho ya siku muhimu kama ya kuzaliwa lakini kuna umuhimu gani kama siku hiyo inabaki kuwa "siku muhimu" tu pasipo kuangalia wapi umetoka,ulipo na unakoelekea?

Na katika mantiki hiyohiyo,Siku ya Wapendanao inakuwa tu na umuhimu kama upendo utatafsiriwa kwa dhamira na vitendo.Kuna umuhimu gani wa kuadhimisha Siku ya Wapendanao kwa kadi za gharama na vinywaji ilhali umewasahau wanaohitaji upendo wako?

Wengi tunaelewa namna baadhi ya wenzetu wanavyoiogopa siku hii kutokana na kuwa na ma-Valentine wengi.Na miongoni mwa hawa ni wale wanaoadhimisha siku hii na "nyumba ndogo" huku wakiacha visingizio kwa wapenzi wao halisi.Hali hiyo inapoteza maana nzima ya siku hii.Haiwezekani mtu kudai anaadhimisha Siku ya Wapendanao kwa kumsaliti mpenzi wake.

Vinginevyo,nawatakia Siku njema ya Wapendanao nikiamini kuwa maadhimisho ya siku hii yatakuwa ya dhamira zaidi kuliko vitendo pekee.

10 Feb 2009

Pengine mie mshamba.Huenda ndio matokeo ya kutozaliwa Ocean Road hospital i.e. "kuja mjini ukubwani".Au labda huu ndio "ukale",au tuseme "kutokwenda na wakati."Lakini nabaki kuwa mmoja wa watu wanaoiona tarehe 14 ya mwezi Februari,Valentine's Day-Siku ya Wapendanao-kuwa siku ya kawaida kama siku nyingine katika mwaka.Na nisemapo "siku ya kawaida" simaanishi tu kwamba ina masaa 24 kama siku nyingine bali pia napigilia msmari kwenye umuhimu wa siku yenyewe.

Kwangu,na kwa misingi yangu ya Uafrika,kumpenda mwandani wangu ni suala la kila siku.Napojimudu kumnunulia zawadi,basi hilo ni suala la kila wakati pasipo kutegemea mwezi au majira.Kwangu,siku ya wapendanao ni kila siku niliyo kwenye mapenzi ya dhati.

Sina takwimu sahihi kuhusu Siku ya Wapendano huko nyumbani lakini nachokumbuka ni kwamba ilianza kuchukua kasi sambamba na zama za mageuzi katikati ya miaka ya 80 (mid-1980s),mageuzi yaliyopelekea mabadiliko kwenye nyanja za siasa,uchumi,jamii na utamaduni.

Sina ugomvi na wanaoienzi siku hiyo,hususan wale walio kwenye mapenzi ya dhati,lakini nina walakini na wale wanaoigeuza siku hiyo kama fursa ya utapeli wa mapenzi (ntafafanua) na commercialization ya siku yenyewe.Naam,siku hiyo hutumiwa na baadhi ya matapeli wa mapenzi "kuthibitisha" mapenzi yao kwa watapeliwa.Iko hivi:unaye-spend nae Siku ya Wapendanao ndio mpenzi wako wa dhati (unaweza kubisha lakini ndio kanuni zisizo rasmi za siku hiyo huko mtaani).Matapeli wanaweza kuzungukia nyumba ndogo zote na kuishia kulala na aidha mama watoto au nyumba ndogo kuu.Uzoefu unaonyesha kuwa wake/mama watoto ni victims wakuu wa Valentine's Day,ambapo waume kudanganya kuhusu semina za dharura nje ya mji au udhuru wowote utakaomwezesha mume tapeli kulala nje,ni mambo ya kawaida.Ndio maana katika siku hiyo baadhi ya akinamama huwawakia waume zao wanaozuga kuleta rundo la maua na kuwauliza "badala ya kuleta vichanja vya mchicha,wewe unatuletea hiyo mimaua...je tutakula ugali na maua?"Sio kwamba wana hasira na maua,bali umuhimu wake unakuwa umepotezwa na matendo kati ya tarehe 15 ya mwaka uliopita hadi mkesha wa Siku ya Wapendanao.
Takwimu zisizo rasmi (au ziite za kimbeya) zinadai kwamba ni rahisi zaidi kwa kabwela kupata chumba cha kupanga mwaka mzima huko Masaki,Oysterbay,Mikocheni na sehemu nyingine za "kishua" kuliko kupata chumba cha usiku mmoja tu kwenye guest houses katika Valentine's Day (labda booking iwe imefanyika mapema zaidi).





Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.