18 Mar 2011

Ama kweli ndoto zimepata muotaji.Yaani ukisikia baadhi ya ndoto za mtu aliyekabidhiwa kuongoza Watanzania zaidi ya milioni 40-namaanisha Rais Jakaya Kikwete-unaweza kuugua ghafla.Ukiweka kando rekodi yake ya kusafiri mno nje ya nchi,Kikwete anaweza kuweka rekodi nyingine ya kuwa kiongozi wa nchi aliyewahi kutoa ahadi nyingi zaidi kuliko yeyote yule duniani.Na rekodi hiyo inaweza kupata ushindani kutoka kwa nyingine ya "Mwanasiasa aliyetoa ahadi hewa nyingi zaidi kuliko yeyote yule.

Sasa amekuja na ahadi mpya ya kuwaunganisha wanafunzi mpango maalumu wa kutumia mkongo wa mawasiliano, ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika shule za sekondari nchini.Katika kufanikisha "mpango huo kabambe", shule zote za sekondari zitaunganishwa katika mtandao huo ambao utawawezesha mwalimu mmoja kufundisha shule hizo wakati mmoja.


Wazo zuri lakini ni la kidanganyifu.Kama serikali ya Kikwete inasuasua kumudu ujenzi wa vyoo katika shule,achilia mbali madawati,madarasa na nyumba za walimu,hizo ndoto za kuwezesha teknolojia ya kisasa anayoizungumzia inatoka wapi?


Na kwa mgao huu wa umeme unaosababishwa na ufisadi ulioshamiri kweye sekta ya nishati,hiyo teknolojia ya mkongo itatumia nishati ya kuni,maji au majini ya Sheikh Yahya (kama bado hayaja-expire)?



Hivi nani amemwambia Kikwete kuwa akikaa kimya-badala ya kutoa ahadi zinazotokana na ndoto za mchana-urais wake utakuwa mashakani?


Hebu jisomee mwenyewe uzushi huu

JK: Tutatumia mkongo kufundishia wanafunzi 
Thursday, 17 March 2011 20:27

Fredy Azzah
RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali imebuni mpango maalumu wa kutumia mkongo wa mawasiliano, ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika shule za sekondari nchini.Katika kufanikisha jambo hilo, shule zote za sekondari zitaunganishwa katika mtandao huo ambao utawawezesha mwalimu mmoja kufundisha shule hizo wakati mmoja.
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Januari mwaka 2006 na kutoa maagizo ya kuboresha elimu kwa miaka mitano ijayo.

"Pamoja na kuwa tuna tatizo la upungufu wa walimu kwa jumla, hali ni mbaya sana kwa walimu wa sayansi, mpaka sasa kuna upungufu wa walimu 34,000 na sisi kwa mwaka uwezo wetu ni kuzalisha walimu 10,000," alisema Rais Kikwete.

Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali itaziunganisha shule za serikali katika mkonga wa taifa wakati ikiendelea pia kuzalisha walimu kadri itakavyoweza."Kutokana na idadi ya walimu wanaosoma, tatizo la walimu litaweza kwisha baada ya miaka mitatu, lakini sasa pamoja na walimu 10,000 kumaliza masomo yao kwa mwaka, unaweza kukuta bado tuna upungufu wa walimu 40,0000 kwa mwaka," alisema

"Tukiziunganisha shule zetu kwenye mkongo wa taifa ambao mpaka kufikia Juni mwaka huu utakuwa umekamilika, mwalimu mmoja akiwa hapa, anaweza kufundisha wanafunzi wa kemia nchi nzima kwa wakati mmoja." alisisitiza.

Alisema mpango huo ukifanikiwa mwalimu atakaye kuwa yupo kwenye darasa la shule husika, kazi yake itakuwa ni kusimamia wanafunzi kufanya mazoezi na yatakayotolewa na mwalimu aliyekuwa akifundisha kwa njia ya mtandano na kusahihisha kazi zao.

Alieleza kuwa, tayari serikali imeshafanya mazungumzo na kampuni moja ya Kimarekani ambayo itasaidia katika teknolojia hiyo."Wameshanionyesha jinsi tutakavyofanya kwenye maeneo ambayo yana umeme na hata yale yasiyokuwa na umeme," alisema Rais Rais pia aliitaka wizara kuweka bayana mipango yake kuhusu namna ya kuinua ubora wa elimu.

CHANZO: Mwananchi

2 comments:

  1. na sio hiyo tu - waziri, Mhe Eng. Dr Kawambwa, alimwakikishia kuwa "the ministry was currently implementing a programme known as 'TANZANIA BEYOND TOMORROW (TBT)' that seeks to employ Information and Communication Technology (ICT) in secondary and primary education." (Daily News).
    sasa kichekesho, kama ulivyobainisha vizuri kwa picha, Tanzania haijaishi hata hiyo JANA , itazungumzaje kuishi KESHO KUTWA. Ninajua hii kaulimbiu ya "TOMORROW" sasa hivi inatumiwa sana hasa katika jamii za magharibi katika kampeni za kuchangisha fedha za kuboresha taasisi za kielimu. Sasa hapa kwetu tumeona hao wanatuzidi nini kusema "TOMORROW" kama tunaweza kusema "BEYOND TOMORROW" - alimradi!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. jk hajitambui na ccm yake ndo kabisa watoke watuachhie nci yetu

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.