7 Apr 2011


Wakenya wanne wanaodai waliteswa na utawala wa kikoloni wa Uingereza katika jitihada zake za kukandamiza harakati za kundi la Mau Mau,wamefungua kesi jijini London.

Kundi hilo linalodai fidia katika mahakama kuu ya hapa linadai kuwa walishambuliwa na maafisa wa serikali ya kikoloni ya Uingereza nchini Kenya kati ya mwaka 1952 na 1961.

Maelfu ya wanaharakati wa Mau Mau waliwekwa kwenye kambi za wakoloni hao na kuteswa huku wengine wakiuawa,wanasema wanaharakati hao.

Serikali ya Uingereza inadai kuwa muda mrefu umepita tangu yalipotokea matukio hayo,na hivyo inadai haiwajibiki nayo.

Hatua hiyo ya kisheria inachukuliwa na wanaume watatu na mwanamke mmoja ambao umri wao ni kati ya miaka 70 na 80.

Mawakili wao wanadai kuwa Wakenya hao wanne wanawakilisha sehemu kubwa ya jamii ya Wakenya walionyanyaswa kutokana na ushiriki wao,au kuhusiswa na harakati za mapambano dhid ya wakoloni katika miaka ya 1950s.

"Wizara" ya Mambo ya Nje ya Uingereza (Foreign Office) inakiri kwamba suala la Mau Mau linazua hisia kali na kwamba zama hizo zilisababisha maumivu makubwa kwa pande zote.

Hata hivyo,"Wizara" inaeleza kuwa Uingereza itajitetea kikamilifu dhidi ya madai yaliyomo kwenye kesi hiyo,ikidai kuwa haiwajibiki.

Uchambuzi wa nyaraka zinazohusiana na kesi hiyo umepelekea kugundulika kwa maelfu ya mafaili ya tawala za kikoloni za Waingereza,ikiwa ni pamoja na nchini Kenya,na "Wizara" ya Mambo ya Nje inatarajia kuweka rekodi hizo hadharani.

Harakati za Mau Mau zilianza miaka ya 1950s kwa lengo la kudai ardhi iliyoporwa na utawala wa kikoloni.

Wanahistoria wanadai kuwa harakati za Mau Mau zilichangia katika kupatikana uhuru wa Kenya.

Hata hivyo,harakati hizo pia zilishutumiwa kwa ukatili dhidi ya wakulima wa kizungu na mapambano ya umwagaji damu dhidi ya askari wa utawala wa kikoloni.

Kamisheni ya Haki za Binadamu nchini Kenya imesema kuwa zaidi ya Wakenya 90,000 waliteswa au kuuawa katika kipindi hicho,na watu 160,000 waliwekwa kizuizini katika mazingira ya kuogofya.

Ripoti rasmi iliyochapishwa mwaka 1961 ilidai kuwa zaidi ya Waafrika 11,000,wengi wao wakiwa raia wa kawaida,na wazungu 32 waliuwa katika kipindi hicho.

Habari hii imeandaliwa kutokana na habari kwenye kipindi cha "Breakfast" cha BBC1 Scotland na tafsiri isiyo rasmi kutoka kwenye tovuti ya BBC

1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube