22 Apr 2011


Nina miaka kadhaa sijawahi kwenda kanisani.Sijisifu wala kujisikia vizuri.Kila mara ninapoongea na Baba huwa nalazimika kumdanganya kuwa siku hizi nakwenda kanisani.Ninatoka familia ya kidini hasa,na huenda leo hii ningekuwa padre kama nisingeamini kuwa sina wito.Hata hivyo,familia yetu imemtoa mmoja wetu kwa Bwana,na sasa yeye ni sista.
Mdogo wangu mpendwa,Sista Maria-Solana Chahali

Leo ni Ijumaa Kuu,siku ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili yetu.Nimesema sijatia mguu kanisani kwa miaka kdhaa lakini najitahidi kadri ninavyoweza kuishi kulingana na matakwa ya Bwana.Sio kwenda kanisani au kuimba mapambio kutakompatia mwanadamu uzima wa milele bali matendo.Japo ni muhimu kujumuika na waumimni wenzetu makanisani,la muhimu zaidi ni kuishi kwa mfano wa Bwana Yesu ambaye licha ya upendo wake usiomithilika alikuwa tayari kufa msalabani kwa dhambi zetu ili atuletee ukombozi.

Wakati tovuti hii inakutakia wewe msomaji mpenda Ijumaa Kuu njema,siku hii inaweza kuadhimishwa ipasavyo kwa kutafakari kuhusu upendo wa Bwana,kujitoa kwake kwa jili yetu na upeno kwa ujumla.Kama humpendi jirani yako unayemwona kila siku utakuwa mnafiki kudai unampenda Bwana mbaye hujawahi kumwona.Yesu ni upendo na amani.

4 comments:

  1. Nawe pia na msalimia Sista Maria-Solana.

    ReplyDelete
  2. Asante mdau Malkiory na asante dada Yasinta (nitawasilisha salamu kwa sista).

    ReplyDelete
  3. Huu ni wakati wa kutafakari kusudi hasa la maisha yetu hapa duniani. Maisha yetu yana thamani na lengo muhimu ndiyo maana Yesu Akaja kutufia. Ni wajibu wetu basi kuwasaidia ndugu zetu wanaoteseka na kuwa kiini cha faraja na farijiko kwa wengine hapa duniani.

    Ingependeza kama nini kuona kuwa mafisadi wote wanatoa zaidi ya nusu ya utajiri wao kusaidia masikini katika kipindi hiki tunapokumbuka mateso ya Mkombozi wetu. Ati hayo mabilioni yote yatawasaidia nini siku watakapokuwa kimya katika majeneza yao ya thamani?

    Nakutakia Pasaka Njema kwako wewe pamoja familia yako!!!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.