27 Apr 2011


Hatimaye Rais Barack Obama wa Marekani ameamua kuweka hadharani cheti chake cha kuzaliwa baada ya kuandamwa muda mrefu na wapinzani wake wanaomtuhumu kuwa si mzaliwa wa nchi hiyo.

Kasi ya mashambulizi dhidi ya Obama ilishika moto baada ya mfanyabiashara tajiri anayetarajiwa kuwania nafasi ya Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani,Donald Trump,kuungana na kundi la wahafidhina wanaodadisi u-Marekani wa Obama.Kundi hilo linalojulikana kama Birthers,limekuwa likipiga kelele kwa nguvu kuwa Obama ni Mkenya na si Mmarekani,madai ambayo Rais huyo aliyapuuza kwa muda mrefu lakini hatimaye amaeamua kuyakabili.

Akiongea na waandishi wa habari leo asubuhi,Obama alitanabaisha kuwa "ana mambo ya msingi zaidi ya kushughulikia kuliko upuuzi huo (kuhusu uhalisi wa uraia wake)".

"Hatutoweza kufanikiwa iwapo tutayumbishwa,hatuwezi kufanikiwa iwapo tutatumia muda wetu kuchafuana...kama tunazua tu mambo na kujifanya kuwa ukweli ni uongo,hatutoweza kutatua matatizo yetu kama tutawaendekeza wazushi",alisema Obama ambaye alizaliwa Agosti 4 mwaka 1961 huko Honolulu,Hawaii kwa baba Mkenya na Mama Mmarekani Mweupe.

Hata hivyo,dakika chache baada ya cheti hicho cha kuzaliwa kuwekwa hadharani,Trump aliendeleza mashambulizi yake kwa Obama akidai cheti hicho-ambacho bado anakitilia mashaka-kisingwekwa hadharani bila mashambulizi yake kwa Rais huyo.Kadhalika,kundi la Birther limeendelea kuonyesha wasiwasi wake huko baadhi ya wanakundi wakidai cheti hicho ni cha kufoji.

Lakini pengine kwa kugundua kuwa suala la uraia wa Obama halina msingi,Trump alisharukia ajenda nyingine akihoji elimu ya Rais huyo.Tajiri huyo mpenda sifa anamtuhumu Obama kuwa alikuwa "mwanafunzi kilaza" (asiyejimudu kitaaluma) na hakustahili kujiunga na Vyuo Vikuu vye hadhi na heshima kubwa (Ivy League) vya Columbia na Shule ya Sheria ya Harvard.

“Inakuwaje mwanafunzi mbovu anakwenda Columbia kisha Harvard?"Trump alimuuliza mwandishi wa habari wa Associated Press. “Natafakari kuhusu suala hili,na kwa hakika nitalichunguza.Atuonyeshe rekodi zake.” Aliendelea kudai, "kuna maswali kadhaa ambayo hayajajibiwa kuhusu rais wetu".

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanadai kuwa inawezekana Tump ana sukumwa na hisia za ubaguzi wa rangi katika mashambulizi yake dhidi ya Obama,huku kebehi zake dhidi ya elimu ya Obama zikitafsiriwa kama "watu weusi hawastahili kwenda vyuo bora nchi Marekani.



VYANZO: Habari hii imetokana na vyanzo mbalimbali mtandaoni hususan jarida la mtandaoni la Huffington Post.

2 comments:

  1. yaani this imenigusa till my heart....soo wrong to ask the blak guy for his birth certificate to prove is he is an AMerican citizen...isnt one of the qualifications of runnin for American president that u must be an American...ssaa wats the hold up...I hate Donald Trump

    ReplyDelete
  2. Me too.Used to admire the Trup lakini katika hili,amejidhihirisha kuwa he's just one of the racist right-wing scums.However,hii ishu inaweza ku-backfire na Trump akaishia kupoteza credibility.

    Thanks for the comment

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.