5 Apr 2011


Balozl Peter Kallaghe

JUMUIYA YA WATANZANIA-TANZ-UK ikishirikiana na TA Reading Inapenda kuwakumbushia tena  watanzania wote waishio Reading, Slough, Oxford na vitongoji vingine,  Kuwa  Ziara ya Balozi wetu MH Peter Kallaghe akiambatana na Mama Kallaghe Itaanza rasmi siku ya Ijumaa jioni tarehe 8/4/11 na kuendelea Tarehe 9/4/11 Jumamosi ambapo Mh. Balozi Kallaghe atakutana na Jumuiya mbali mbali za Ki-Tanzania, pamoja na kutembelea miradi na Taasisi mbali mbali za KiTanzania.

Wakati Huo huo Mama Kallaghe atajumuika na na akina mama wote Jumamosi kuanzia saa nane Mchana. Kisha Mh Balozi na Mama Balozi watahudhuria hafla kubwa iliyoandaliwa na Wanajumuiya kwa ajili ya kuwakaribisha kuanzia saa kumi na mbili jioni.  Bongo DJs watakuwepo wakifanya makamuzi  mpaka usiku wa manane.  Jumapili 10/4/11 kutakuwa na ibada ya Kiswahili itakayohitimisha Ziara hii ya kipekee.

Kutokana na muitiko mkubwa pamoja na ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa wanajumuia imelazimu kubadilisha ukumbi ili kufanikisha zaidi ziara hii.  Anuani ya Ukumbi Rasmi itakuwa WYCLIFFE 233 KINGS ROAD, READING RG1 4LS. Tunawaomba Radhi  wote kwa usumbufu uliotokana na mabadiliko hayo muhimu. Tafadhali mjulishe mwenzako na tuzingatie mda.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu ziara hii tafadhali wasiliana na wafuatao: Ndg. Hussein 07865673756, Ngd. Upete 07796122127, Mama Maria 07919874182.

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu.

TANZ- UK / TA READING

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.