9 May 2011


Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuonekana kituko kwa kupokea hundi yenye tarakimu zinazokinzana na thamani ya hundi hiyo kwa maandishi,na yeye kuonekana akitoa tabasamu la nguvu (trademark yake),sasa imekuwa zamu ya mkewe.

Ukiangalia hundi anayokabidhiwa Mama Salma Kikwete (pichani juu) utabaini kuwa thamani ya hundi kwa maandishi ni shilingi milioni tatu na laki nane,ambayo kwa tarakimu inapasa kuwa 3,800,000.Sasa sijui ni umaimuna au uzembe tu,tarakimu za hundi hiyo zimeandikwa kichakachuaji- TZS 3,800,00.Unaweza kudhani ni shilingi elfu tatu mia nane (3,800.00) lakini maelezo ya hundi yatakusuta kwani yametamka bayana kuwa ni SHILINGI MILIONI TATU NA LAKI NANE.

Na hapa chini tunamwona mtu tuliyemkabidhi dhamana ya kutuongoza Watanzania takriban milioni 50 akikenua meno kwa furaha huku hundi imeandikwa TWO HUNDRED THOUSAND lakini tarakimu ni 300,000Hivi kabla ya hafla hizi, hao jamaa wa  PSU  hawakagui vitu anavyokabidhiwa Rais au mkewe?Au nao hadithi ni hiyohiyo?

Na haya ni madudu nadra tunayobahatika kuyaona hadharani.Je yanayofanyika kwa kwa faragha ua sirini inakuwaje?Npatwa na wasiwasi kuwa hadi Kikwete anaondoka madarakani hapo 2015 (kama hatoombwa na mafisadi kugombea tena ili aendelee kuwalinda) tunaweza kushtukia Tanzania ishauzwa zamani hizo.Unashangaa nchi inawezaje kuuzwa?Waulize "Zaire" (DRC Kinshasa)!!!!

Chanzo: Nimkutana na habari hii kwa ndugu yangu MPAYUKAJI MSEMAOVYO

2 comments:

  1. This is a jokeeeeeeeeeee lol

    ReplyDelete
  2. hayo sio matatizo ya viongozi hayo matatizo ya watu waliongozana na raisi ambao wao ndio wanalihakikisha kwanza kabla kufika kwa kiongozi sawa,hao walinzi wake wanafanya nini?na ndio wenye hilo kosa,wao wakihahakisha ndio wanaruhusu kukabidhiwa raisi,mdau bwegenaz

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube