16 May 2011


Rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kushangaa hajambo.Sasa anashangaa kwanini kuna utitiri wa mabango yenye ujumbe dhidi ya rushwa lakini rushwa inaendelea kutawala katika wizara mbalimbali bila uoga.

Tell you what Mr President,jibu la kinachokushangaza ni rahisi sana.Kama wewe mwenye kila nyenzo ya kukabiliana na rushwa,na ambaye ulitangaza hadharani kuwajua wala rushwa ila uliwapa muda wa kujirekebisha-na wakagoma kujirekebisha,lakini unaogopa kuwachukulia hatua-unasuasua katika kutekeleza ahadi uliztoa mwenyewe,unatarajia nini kutoka kwa watu wasio na uwezo wala mamlaka ya kupambana na rushwa?

Wewe unashangaa na sie tunakushangaa pia.One thing for sure,rushwa haiwezi kumalizwa kwa Rais kushangaa.Kinachohitajika ni vitendo na sio kubembelezana katika semina elekezi zinazozidi kuwatwisha mzigo walipa kodi masikini.

Jaribu kuwa mkali kidogo,punguza kushangaa,fanya vitendo.

Habari kamili ni hii hapa chini

Kikwete ataka vita vya rushwa kwa vitendo

na Danson Kaijage, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza mabango yote ya kupambana na rushwa yanayobandikwa katika wizara na taasisi za serikali na za umma yaendane na matendo yanayofanywa na maofisa katika ofisi husika.

Alitoa agizo hilo jana alipokuwa akifunga semina elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali iliyofanyika mjini Dodoma kwa siku saba.

Alisema wananchi wangependa kuona ukusanyaji wa mapato unaimarika na nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za umma inakuwa bora zaidi badala ya kujaza mabango mengi yasiyokuwa na faida.

Alisema wananchi wanatarajia kuona juhudi za mapambano ya kweli kwa kudhibiti mianya ya rushwa badala ya kuona mabango mengi bila kuwepo na juhudi za makusudi.

Rais Kikwete alisema kinachoshangaza ni kuona wingi wa mabago katika kila kona wakati rushwa inaendelea kutawala ndani ya wizara mbalimbali bila woga.

Aidha, alisema kutokana na kuwepo kwa rushwa kuanzia ngazi ya juu ni wazi kuwa rushwa itaendelea kutendeka hadi ngazi ya chini kwa kuwa misingi ya rushwa inaanzia ngazi ya juu na kushuka ngazi ya chini.

Aliwataka vingozi na watendaji wakuu hao, kuonyesha ujasiri mkubwa juu ya kupiga vita masuala ya rushwa badala ya kuoneana aibu na kufichiana siri.

Rias Kikwete alisema semina hiyo ambayo ilikuwa na mikakati ya kuimarisha utendaji ndani ya serikali inapaswa kuzaa matunda hasa katika mapambano dhidi ya rushwa.

Hata hivyo, alisema wananchi wanatazamia kuona viongozi wa ngazi ya juu wakiwa mfano mzuri wa utawala bora, kuheshimu Katiba, utawala wa sheria na nidhamu ya kazi na uwajibikaji.

Naye Katibu Mkuu Kiongozi, Philimon Luhanjo, alisema waliazimia mazimio 14 ambayo viongozi hao wanatakiwa kuyatekeleza na kuyawasilisha katika ofisi yake kila baada ya miezi mitatu.

Semina hiyo iliwashirikisha mawaziri, makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.1 comment:

  1. Hayo ya rushwa awaachie TAKUKURU. Alitakiwa kuzungumzia ufisadi ambao ndio unaratibiwa na hao wateule wake. Hapo ningepata matumaini kidogo kuwa ameanza kutekeleza falsafa yake ya 'kujivua gamba'.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube