18 May 2011


Hasheem Thabeet afanya.....

Na Brighton Masalu

STAA wa mpira wa kikapu, duniani akicheza katika Ligi ya NBA nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka ‘Super Tall’ (pichani) amefanya kufuru ya fedha baada ya kumwaga fedha ukumbini na kuwaacha watu wagombanie, twende mstari kwa mstari.

Paparazi wa gazeti hili lenye heshima ya nyota tano kwa habari za mastaa Bongo, alishuhudia tukio hilo live wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, jijini Dar es Salaam ambapo handsome boy anayecharaza fimbo katika muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ alikuwa akipiga shoo babkubwa.

Awali kasuku wa gazeti hili alimshuhudia Hasheem akikatiza kwa madaha ukumbini humo, akiwa ameongozana na wapambe wake waliokuwa wakimuandalia njia, kisha kukaa sehemu moja na kuanza kula bata kwa mtindo wa ‘tingisha kama imeisha, leta nyingine’.

Wakati shoo ikiendelea Hasheem aliinuka na wapambe wake kuongoza mbele kama kawa, kisha wakaelekea jukwaani alipochomoa burungutu moja la ‘nyekundu nyekundu’ tupu na kumkabidhi Dully Sykes ambaye aliongeza manjonjo baada ya kutuzwa na supastaa huyo.

Hakuishia hapo, aliposhuka jukwaani, alizama mfukoni na kutoa burungutu lingine kisha akalirusha juu na mashabiki kuanza kugombania.

Wakati watu wakiendelea kukanyagana wakigombea mkwanja huo wa ‘sadakalawe’ Hasheem na wapambe wake walitoka nje na kuingia kwenye gari aina ya Hummer na kuondoka kiwanjani hapo.

“Duh! Ebwana ee, jamaa huyu ni noma yaani minoti yote hiyo kaiachia watu wanyang’anyane? Hii ni kufuru, kweli mshkaji fedha imemkubali,” alisika jamaa mmoja akisema ukumbini hapo.

Hasheem Thabeet amerejea nchini hivi karibuni akitokea Marekani anapoishi, yupo kwa mapumziko mafupi. Ni Mtanzania pekee anayeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye ligi ya NBA ya mpira wa kikapu nchini humo.

Na yafuatayo ni maoni ya wasomaji wa gazeti hilo

Comment by Eddie Mourice Junior 1 hour ago
Kwa hili umechemka hasheem even if ur money!
Comment by KUU LA MAADUI 7 hours ago
Dogo pesa ni zako lakini kwa hii ya leo umetimba ,sikujua kama na wewe bado mgeni na pesa aise kwa nini unafanya hivyo hujui kama anaweza kufa mtu katika kugombania minoti halafu wewe ukastakiwa kwa kusababisha vifo ,aise umeniuthi unakuwa mrefuuu 22222222 nje ndani mfupi acha ulimbukeni najua hata ndugu zako hawata fuhia upuuzi huo,kama unapesa unakuwasha utumie katika mambo mazuri mungu atakubariki sio kurushia walevi.
Comment by Minja Frank 7 hours ago
Ona mwenzio mwenye kipaji cha mpira wa kikapu kama wewe Dikembe Mutombo wa DRC kajenga Hospital kubwa tu Kinshasa. Wewe wamwaga pesa yako kwenye masanga. Saidia nchi yako!!!
Comment by Alphoncene Gerald 8 hours ago
Sina hata cha kuchangia
Nachoka kabisa
Comment by Miriam John Mndolanga 8 hours ago
Ulivyofanya ndivyo nafsi yako ilivyokutuma, kwa upande wako ni sawa tu ila ni vema hela unayoitolea jasho na kusumbuka sana hadi kuipata ungeiwekeza kwa makundi yenye mahitaji maalum na Mungu atakubarikia zaidi ya ulichotoa. Jifunze kupitie kwa waliofanya kama hivyo wameishia wapi?
Badilika Hasheem, usijijengee sifa mbaya kwa jamii yako.
Comment by julius manning 8 hours ago
huo ni ulimbukeni mkubwa akumbuke akina Tyson walikuwa na hela kuliko yeye lakini leo je
Comment by swalih/waziri 8 hours ago
huo niulimbukieni wakati familia nyengine pesa yakula mtihani wewe pesa unazigawa kwa walevi inshlwa mungu akulaani uje kuzikumbuka sikatowe misaada makanisani msikitini na mashuleni wewe unagawa kwa walevi ili upate jina kuwa umegawa pesa<.
Comment by Matu 8 hours ago
Pesa ni sabuni ya roho lakini pesa nazo zina upepo wake...wakati ukuta...pesa ni kama maua..huchanua na kusinyaaa kwa mtoto wa manka sasa zimechanua...!
Comment by anna [email protected] 8 hours ago
Ama kweli masikini akipata matako huria mbwata, hivi wewe umesahau tabu zote ulizopita, haya baba wakati wako hivi humuoni mwenzio yule modo anaitwa matata kila mwaka anatoa msaada kwa yatima wewe unagawa pesa kwa walevi, una akili nyingi sana mtoto wewe, ina maana hata kule kijijini kwenu huna wanaohitaji msaada, utakuja juta baadae na hao wapambe huta waona sana watakucheka, wapi nice??? unalewa sina
Comment by ikk 8 hours ago
Kweli minoti unaigawa kwa watu wenye ziada tele, tena Klabu? Wakati kuna watoto yatima huko makete wanalea wadogo zao, tena kwa kupika pombe za kienyeji?
Laana huanza polepole!
Comment by Sebastian Salatiel Shemhilu 9 hours ago
DUUH!! HII NI DHARAU YA FEDHA AU JEURI YA FEDHA? HASHEEM TOA PESA ZAKO KWA YATIMA KULIKO KUWAPA PESA WALEVI NAMNA HIYO.MUNGU ATAKUPA ZAIDI.

Comment by Mapresha Getebariadi 9 hours ago
Hela iko wapi wenye fedha hawafanyi hivyo hapo alikuwa anawachanganya warembo waanze kujimwaga kwake. Kama anahela si asomeshe hata yatima 2 tu.
Comment by edmas 9 hours ago

Haya bana, wakati wako huu. Alikuwepo Mr. Nice naye alifanya kufuru ya pesa, sasa yupo apeche alolo, kushnei.
Comment by furaha Tausi 9 hours ago
WEE HASHEEM WEWE KWANINI HIYO HELA USIWASAIDIE HATA WATOTO WA MITAANI JAMANI HATA WALE WATOTO WALIOKO OCEAN ROAD HOSPITAL WANAUMWA KANSA?? MUNGU ATAKULAANI SHAURI YAKO

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.