12 May 2011Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti mahiri la Raia Mwema inakwena kimataifa na kuangalia kifo cha Osama bin Laden;alipotoka na kujiimarisha,na kufanya tafakuri ya hatma ya usalama duniani baada ya kifo cha gaidi huyo.Kadhalika,najaribu kumkumbusha Rais wetu Jakaya Kikwete juu ya umuhimu wa ahadi thabiti.Obama alipoingia madarakani aliapa kumsaka Osama kwa udi na uvumba,na hatimaye akafanikiwa (japo hakuwa na hakika gaidi huyo yuko wapi).Kikwete alipoingia madarakani alitanabaisha kuwa anawafahamu wala rushwa kwa majina lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Sote tunajua kuwa sio tu hawajajirekebisha bali wamempuuza mkuu huyo wa nchi.Imagine Obama angempa Osama muda wa kijisalimisha...!!!

Pamoja na makala hiyo ni makala nyingine mwanana na habari za kina ndani ya jarida hili nambari wani.BONYEZA PICHA HAPO JUU KUSOMA MAKALA HIYO PAMOJA NA HABARI NA MAKALA NYINGINEZO

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube