20 Sept 2011



Mdau mmoja mkubwa wa blogu hii amenitumia ujumbe ufuatao,nami naomba niuwasilishe kama ulivyo 


20/09/2011 09:00 kaka chahali.....naheshimu sana kazi zako za uandishi....ila kwahili nahisi umekosea

nikweli magamba wanafanya kila wawezalo huko igunga ila kutumia picha isiyo na uhalisia juu ya tukio hilo ni jambo la kudhalilisha taaluma yako ya uandishi.....

Picha ya kwanza ni imepigwa morogoro na si igunga na tena ilikuwa ni mashindano ya kula .....verify it here http://issamichuzi.blogspot.com/2011/07/mashindano-ya-kula-yafana-sana-mkoani.html

chonde ni heri kutoa habari bila picha kuliko kucopy and paste picha za matukio mawili tofauti....

ningefurahi kama utalitolea ufafanuzi jambo hili....

Regards,KM
mdau ninayefatilia kazizako twitter,facebook na kwenye hii blog yetu tuk


Baada ya kufuatilia kiungo (link) kilichobainishwa na mdau huyo nimegundua kuwa chanzo cha picha husika (ambacho ni jukwaa la mtandaoni la Jamii Forums) hakikuwasilisha picha husika kwa usahihi.

Naomba kutumia fursa hii kuomba radhi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wote walioguswa na picha husika.Kuna nyakati waandishi hujikuta katika wakati mgumu kuthibitisha uhalisia wa kila habari,picha au chanzo cha habari/picha husika.

Lakini ni matumaini yangu makubwa kuwa kila msomaji wa blogu hii ataiga mfano wa mdau MK pindi kunapojitokeza mapungufu au makosa ya aina yoyote ile.Kwangu,kukosolewa ni miongoni mwa njia za kujifunza na kujirekebisha.Naomba kumshukuru sana mdau MK kwa ujumbe wake,na ninatumini tutazidi kushirikiana.

2 comments:

  1. Kinachonishangaza ni je, kwa nini CCM haikujitokeza rasmi na kutoa ufafanuzi tangu pale mwanzo? Hawana kitengo cha mawasiliano na umma? Hawana msemaji anayewajibika kufafanua masuala ya chama na kuwaelimisha wananchi?


    Blogu ya Kulikoni, kama ilivyo kwa blogu nyingi, inasomwa na wengi. Je, CCM wanaweza kusema hawakuiona taarifa hii? Na kama waliiona wakakaa kimya, tuwaeleweje? Na je, watu wa namna hii, wasiojali heshima ya chama chao, tuwaeleweje?

    Masuali yangu hayajaisha. Je, je CCM hawaelewi kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa sahihi? Walipoona upotoshaji, kwa nini wasingesahihisha, ili kuheshimu haki ya wananchi ya kupata taarifa sahihi?

    Inakuwaje sahihisho litoke kwa mdau ambaye hata hatuna taarifa zake? Je, haingekuwa busara kwa msemaji rasmi wa CCM kuleta hilo sahihisho, akiwa amejitambulisha kikamilifu na wadhifa wake katika CCM? Kama CCM wanashindwa kushughulikia jambo rahisi kama hili, je mambo makubwa?

    ReplyDelete
  2. Kaka Chahali,nashkuru kwakulitolea tamko jambo hili pia sitegemei kama linaweza kujitokeza tena maana binafsi naamini sana vyanzo vyako na uchambuzi wako wa habari usio jali hisia binafsi

    Mzee wangu Mhe.Mbele : naomba nitofautiane na wewe ktk hoja yako ya msemaji ramsi...kukemea upotoshaji wa habari tena yenye madhara kwa jamii si jambo wala jukumu la msemaji rasmi wa chama peke yake.

    Tusiwe wepesi kuwalaumu magamba na watendaji wake wasiojua wajibu wao bila kujiangalia nafsi zetu "Ulipoona upotoshaji, kwa nini usingesahihisha, ili kuheshimu haki ya mwananchi mwananchi mwenzako ya kupata taarifa sahihi?....

    Let's do our part and the rest is history hata wasipolitolea tamko ila sisi tumesimama kidete na kutetea ukweli wa jambo...

    Mfano raisi,ukimkuta mtoto wa jirani anafanya uovu hauta mkanya eti kisa we si baba yake??la hasha !

    Mhe.Mbele swali unalojiuliza la Je CCM hawaelewi kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa sahihi halina mashiko kwasababu na wewe huku tetea Ukweli bila kujali itkadi za chama au hisia binafsi....

    Sina nia mbaya,ila nimeshangazwa pale tunapokuwa na spirit yakungoja kila kitu ilhali tunaweza kukemea.

    NB:I stand to be corrected


    Regards,
    KM

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.