Anyway,lengo la post hii sio kuzungumzia udhaifu wangu wa namba wala kuelezea kuhusu shule yangu bali ni swali linalonisumbua kuhusu kinachoendelea katika sehemu nyingi za nchi zilizoendelea ambapo kumekuwa na upinzani mkali dhidi ya uroho wa taasisi za fedha (mabenki,nk).
Lakini pengine kabla ya kuelekea huko,swali la msingi linaweza kuwa hili.Inakuwaje nchi kama Ugiriki ikumbwe na msukusuko wa kiuchumi ilhali akina sie (Tanzania) tunaonekana kama "tunapeta" tu?Pamoja na Ugiriki,nchi nyingine ambazo zinasumbuliwa na kuyumba kwa uchumi ni pamoja na Hispania,Ureno,na Italia (ambazo pamoja na Ugiriki zinaunda kinachoitwa PIGS-Portugal,Italy,Greece na Spain).
Hebu wachumi nifahamisheni.Hivi hao PIGS si wapo bora zaidi kiuchumi ukilinganisha na nchi kadhaa za Afrika?Sasa mbona sie tupo kama hakuna tatizo la uchumi?Au sie ni sugu?Au uchumi wetu ni kama haupo?
Halafu kuna hili la harakati dhidi ya uroho wa taasisi za fedha ambazo kwa kimsingi zimeanzia mtaa wa Wall (Wall Street) jijini New York na kupewa jina la Occupy Wall Street,na sasa zinaelekea kusambaa sehemu mbalimbali duniani kama picha zifuatazo zinavyoonyesha.Je,kwanza,kuna uwezekano wa harakati hizo kuhamia nchi masikini?Pili,kwani hazijatugusa hadi sasa?Au ni yale yale ya uchumi usiokuwepo na hivyo kutokuwa na umuhimu wa kuulalamikia?
Nitashukuru sana kama kuna mchumi yeyote atakayeniandikia kwa barua pepe [email protected], kisha nitachapisha hapa,na ninaahidi kuandika makala kwenye jarida la Raia Mwema na kumtaja mchumi mwenye jibu mwafaka
Enewei,hebu tuangalie picha za harakati za "Occupy Wall Street" zilivyosambaa sehemu mbalimbali duniani
 Wall Street,New York,Marekani
 Tokyo,Japan
 Seoul,Korea ya Kusini
 Sydney,Australia
  Sydney,Australia
 Hong Kong
 Zurich,Uswisi
 Seoul,Korea ya Kusini
 Roma, Italia
 Hong Kong
 Frankfurt,Ujerumani
 Roma, Italia
 Stockholm, Sweden
 London,Uingereza
 London,Uingereza
 Sydney, Australia
 Hong Kong
 Julian Assange na waandamani jijini London
 London
London






















0 comments:
Post a Comment