20 Nov 2011


KWA NIABA YA WASOMAJI WA BLOGU HII NINATOA POLE NYINGI KWA BLOGA MWENZETU DINAHICIOUS KWA MSIBA MKUBWA WA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI.

KAMA MTU NILIYEKWISHAPOTEZA MZAZI,NINAFAHAMU KIBINAFSI MAJONZI NA UCHUNGU VINAVYOAMBATANA NA KUPOTEZA MZAZI.KIFO NI KIFO LAKINI CHA MZAZI KINAGUSA SANA.KWA BAHATI MBAYA,HAKUNA MANENO YANAYOJITOSHELEZA KUMFARIJI MFIWA ZAIDI YA KUUNGANA NAYE KWA SALA KUMWOMBEA MAREHEMU APATE PUMZIKO LA MILELE NA MWANGA WA MILELE,APUMZIKE KWA AMANI.

HATA HIVYO,NILIPOFIWA NA MAMA MZAZI MWAKA 2008,PADRE ALIYEONGOZA IBADA YA MAZISHI ALISEMA HAYA: "SOTE TUMELETWA DUNIANI NA MUNGU KWA UPENDO WAKE USIOMITHILIKA.KAMA WANADAMU,TUNAPENDA TUWE PAMOJA SIKU ZOTE.LAKINI BABA YETU ALIYETULETA DUNIANI ANATUPENDA ZAIDI,NA HIVYO ANAWEZA KUTUCHUKUA WAKATI WOWOTE UKE.PAMOJA NA UCHUNGU TUNAOKUWA NAO TUNAPOONDOKEWA NA TUMPENDAYE,NI VEMA KUFAHAMU KUWA JAPO SIE TULIMPENDA MAREHEMU LAKINI BABA YETU (MUNGU) ALIMPENDA ZAIDI NA HIVYO AMEAMUA KUMCHUKUA.NA KWA VILE TUNAJUA ANA UPENDO MKUBWA BASI NA TUPATE FARAJA KUWA HUKO AENDAKO ATAPUMZISHWA KWA AMANI NA UPENDO."

NATAMBUA MANENO HAYA YANAWEZA YASISAIDIE KUPUNGUZA MAJONZI LAKINI YANAWEZA KULETA FARAJA KATIKA KIPINDI CHA MAJONZI YA MSIBA.

POLE SANA DINA,TUPO PAMOJA KATIKA SALA.

PUMZIKO LA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI AMEN

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube