23 Dec 2011


Leon Bahati
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Lewis Makame, ambaye uitumishi wake kwa umma ulimalizika Julai, mwaka huu.

Amemteua pia Julius Mallaba kuwa Mkurugenzi wa NEC ili kuchukua nafasi ya Rajabu Kiravu ambaye naye amestaafu.Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo Jijini Dar es Salaam jana, ilieleza kwamba walioteuliwa walianza kazi tangu Jumatatu iliyopita.

Katika uteuzi huo, Rais Kikwete alimteua Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC.

Kabla ya uteuzi wake, Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.

Naye Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Jaji Omari Makungu.

Kwa mujibu wa Luhanjo, Jaji Makungu aliwahi pia kuteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Luhanjo alisema Mallaba kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

CHANZO: Mwananchi

NAOMBA KUMPONGEZA JK KWA UTEUZI HUU MAKINI.JAJI LUBUVA NI MIONGNI MWWA WATANZANIA WACHACHE WAZALENDO WALIOSALIA.HONGERA SANA MZEE LUBUVA

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.