16 Jul 2013


Proxy War au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili.

Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C.

Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha M23.

Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)

Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa "atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha mtandike" kuna uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC. 

Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23 (wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)

Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."

Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU, ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu (wapelelezi) wa ndani na wa nje.Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50? Soma hapa http://suntzusaid.com/book/13 kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)

Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.

2 comments:

  1. Yah! no comment, Hapo umechambua na upo sahihi kabisa kwa 100%, udogo wa eneo "nchi" ya Rwanda sio kigezo kuwa hawataiweza Tz.
    Especially kuhusu hao wanyarwanda waliopo hapa Tz ni wazo kubwa sana la kuangaliwa

    ReplyDelete
  2. Tanzania Iko fiti kichizi kwenye Uchachero. Wakati tukimboa mataifa ya kusini mwa Afrika nchi ilikuwa makini sana. Ndio maana Makaburu hawakuweza kuimaliza maana wajua wazi kuwa tulifunza Askari wa ukombozi kupambana Msumbiji Namibia Angola Zimbabwe na hata ANC wa Africa Kusini. Wewe Unafiri Id Amin alikuwa lelege lege? Jamaa aliwakunjia Waingereza Akapokea mateka wa Waizraeli Na walipoenda kuokoa mateka akaua baadhi ya makomando wao, And he got away. Lakini Tanzani ikamkongoli yeye na silaha kemkem alizokuwa nazo kutola Libya na Arabuni.
    Kagame nakuonya, tenana nakuonya sana' Find another means of suicide. Acha Ukumbafu!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube