1 Feb 2014

My bad, nimesahau kuweka anwani ya mtandaoni ya RADIO MBAO. Ni www.radiombao.com na itakuwa hewani kuanzia Februari Mosi 2014. Sie tunaamini katika #SharingIsCaring , na RADIOMBAO inakuhamasisha nawe ku-share nasi habari yoyote ile . Usihofie kwamba “ah mie sio mwandishi” tutahariri habari yako na itasomwa/kusikika katika nchi 138 duniani. Na wala usikwazwe na “ah mie sijawahi kuandika” kwani kama unaweza kuandika SMS basi kwa hakika unaweza pia kuandika habari. Pia kila jambo lina mwanzo, mtoto hazaliwi akitembea. Kwahiyo yawezekana RADIOMBAO ikaibua kipaji chako…lakini ili hilo liwezekane basi usihofie ku-share nasi habari. Ni Jumamosi Februari 1, 2014, mahali pa kukutana ni www.radiombao.com #SharingIsCaring  (at Glasgow)

RADIO MBAO: Ninaomba kuwafahamisha kuwa mie na mwenzangu @djkvelli mkongwe wa masuala ya entertainment kama dj nchini Marekani na mmiliki wa kituo maarufu cha radio mtandaoni, RADIOMBAO, tumeunganisha nguvu, na kwa pamoja tunawaletea uzinduzi RADIOMBAO katika sura mpya. Licha ya matangazo ya radio, RADIOMBAO sasa inakuletea habari mbalimbali katika namna tofauti (bringing you news not in your traditional way). Uzinduzi rasmi utakuwa LEO  Jumamosi ya Februari 1 mwaka huu 2014.

 Tunataka nawe uwe mshiriki kwa kututumia habari kwa email [email protected] nasi tutataja jina lako kama utapenda tufanye hivyo. Hii pia ni fursa adimu kwa wasanii kutangaza kazi zenu DUNIANI kwani RADIOMBAO inasikika katika NCHI 138 DUNIANI. Tutatangaza kazi yako ya sanaa BURE. Kwa kuunganisha uzoefu na ujuzi wa muda mrefu wa @djkvelli katika masuala ya entertainment nchini Marekani, na uzoefu wangu wa takriban miaka 10 katika fani ya habari, tunawaahidi kuwaletea kitu kipya,tofauti na kitakachokidhi mahitaji yako ya habari,mahojiano,burudani na soka, maisha najamii, teknolojia na mengineyo mengi. Ombi letu kwako ni kuwa sehemu ya familia ya RADIOMBAO: Mfahamishe ndugu, jamaa na rafiki yako kuhudu ujio mpya wa RADIOMBAO. Karibuni sana kutembelea tovuti yetu inayopatikana katika anwani hii

Wasiliana nasi kwa email [email protected]

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube