 |
Chris Brown akielekea kwenye Lamborghini lake kuondoka katika klabu ya usiku palipotokea shambulio la risasi |
Prodyuza Marion Suge Knight (pichani chini) amejeruhiwa kwa risasi amejeruhiwa kwa risasi katika shambuli lililotokea katika pati iliyokuwa ikiendeshwa na msanii Chris Brown.
Mashuhuda wanaeleza kuwa msanii huyo ambaye bado yupo katika msamaha wa uchungu (parole) baada ya kutoka jela hivi karibuni ndiye alikuwa mlengwa wa shambulio hilo, ambapo alikuwa MC wa pati ya utangulizi wa Tuzo za Video za Muziki (MVA) zitakazofanyika leo usiku (kwa saa za Marekani).
Inadhaniwa kuwa Chris hakuumia katika shambulio hilo, lakini watu wengine watatu, akiwemo Suge Knight, mwanzilishi wa lebo ya muziki ya Death Row Records iliyokuwa ikitumiwa na msanii mwingine maarufu wa nchi hiyo, Marehemu Tupac Shakur, walijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya Cedar's Sinai. Inaelezwa kuwa mmoja wa majeruhi hao yupo taabani.
Mwanamitindo na mcheza filamu Tyson Beckford na memba wa kundi la Black Eyees Peas Apple De Ap walikuwa miongoni mwa waliohudhuria pati hiyo, na walieleza kuwa walisikia sauti nne za risasi mida ya saa 7.30 alfajiri ya kuamkia leo.
 |
Majeruhi akitibiwa |
Suge Knight ambaye kwa sasa anamiliki kampuni ya muziki ya Black Kapital Records alionekana na polisi nje ya ukumbi baada ya shambulio hilo na akachukuliwa katika gari la kubeba wagonjwa. Inaelezwa kuwa alipigwa risasi mbili, na kujeruhiwa tumboni na mkononi na sasa anafanyiwa upasuaji.
 |
Chris Brown 'akijirusha' kabla ya shambulio |
Waliofanya shambulio hilo walikamatwa na polisi ambao sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mastaa wengine waliokuwa kwenye pati hiyo ni pamoja na Justin Beiber na rapa The Game.
 |
Justin Beiber alikuwa miongoni mwa waliohudhuria pati hiyo, kama ilivyokuwa kwa rapa The Game (pichani chini)
 |
Iliposikika milio ya risasi hizo, Chris Brown alionekana akiruka kuelekea kwenye eneo la baa katika klabu hiyo ya usiku (nightclub), huku kwa hasira akiwaagiza watu wengine kujikinga.
 |
Chrsi Brown akiruka kuelekea eneo la baa baada ya milio ya risasi |
Saa 12 kasorobo asubuhi ya leo, msanii huyo alitwiti
Akimaanisha 'Jamii haiwezi kustarehe au kuburudika pasipo mikwaruzo.'
 |
Majeruhi wakiingizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa |
 |
Chris Brown akiwa ametahayari baada ya shambulio hilo
|
0 comments:
Post a Comment