25 Aug 2014

Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola hadi hivi karibuni ulikuwa katika baadhi ya nchi za Afrika Magharibi pekee: Sierra Leone,Liberia, Nigeria, na Guinea. Sasa nchi ya tano imeingia kundini,imeripotiwa kuwa watu wawili wamefariki kwa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC)- zamani Zaire- nchi iliyopo Afrika ya Kati.

Waziri wa Afya wa DRC, Dr Felix Kabange Numbi, ameeleza kuwa watu wawili wamefariki kwa Ebola, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.Kwa mujibu wa ripoti, tayari kuna vifo 13 vilivyosababishwa na ugonjwa huo hatari. Awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilidhani vifo hivyo havihusiani na Ebola hadi ilipothibitishwa na DRC kuwa vimetokana na Ebola.

Uhusino kati ya Ebola DRC na mlipiko katika nchi za Afrika Magharibi hauko bayana, huku WHO ikieleza kuwa bado inaendelea na uchunguzi, hasa kubaini iwapo dalili za 'Ebola ya DRC' ni sawa au tofauti na ile ya Afrika Magharibi.

Hadi mwaka huu, milipuko iliyopita ya Ebola ilikuwa Afrika ya Kati, huku DRC ikiwa mhanga wa mara kwa mara. Kwa mara ya kwanza, Ebola iligundulika eneo hilo mwaka 1976

Je Ebola itaibukia wapi kwingine?

Hadi sasa kumekuwa na matukio yanayohusishwa na Ebola katika bara la Ulaya, Asia na Amerika ya Kaskazini, lakini katika matukio yote, wagonjwa walipimwa na kugundulika hawajaambukizwa ugonjwa huo. Wataalam wa afya hawana hofu ya Ebola kusambaa katika nchi zilizoendelea, kwa sababu milipuko ya ugonjwa huo hujitokeza zaidi katika nchi zenye maji yasiyo salama na zisizo na raslimali za kupambana nao, na sio mataifa tajiri kama Marekani.

Kwa sasa, uwezekano mkubwa wa kusambaa kwa Ebola katika maeneo ambayo hayajaathiriwa ni watu wanaosafiri kutoka eneo moja hadi jingine.Kwa kiwango cha nchi, uwezekano mkubwa wa kusambaa kwa ugonjwa huo ni kwa safari za ndege.

Hadi kufikia Agosti 22  mwaka huu kuna matukio 1082 ya Ebola na vifo 624 vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo hatari 

Imetafsiriwa kutoka tovuti ya kituo cha runinga cha VOX

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.