9 Aug 2014

Klabu Bingwa ya Soka hapa Scotland, imepewa ushindi wa bure katika hatua ya awali kuelekea michuano ya soka Ligi ya Mabingwa (Champions League) barani Ulaya, licha ya kutwangwa bao 6-1 na Legia Warsaw ya Poland.

Celtic walifungwa mabao 4-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Warsaw, Poland, kabla ya kupewa kipigo kingine cha mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika Edinburgh hapa Scotland.

Hata hivyo, timu hiyo ya Poland imeadhibiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kwa kunyang'anywa ushindi na kutolewa mashindanoni kwa kuchezesha mchezaji asiyestahili, na badala yake Celtic wamepewa ushindi wa mabo 3-0, na sasa watachuana na Maribor ya Slovenia.

Hii ni mara ya pili kwa mabingwa hao wa Scotland kuangukiwa na bahati kama hiyo. Mwaka 2011, timu hiyo ilirejeshwa katika Ligi ya Europa licha ya kutolewa kwa mabao 3-1 na timu ya Sion ya Uswisi. Kama ilivyotokea hivi, sasa, kosa la Sion lilikuwa kuchezesha wachezaji wasiostahili

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube