9 Aug 2014

Kwanza ninaomba kukiri kuwa habari nyingi katika blogu hii kuhusu apps zinahusu jukwaa (platform) la Android. Hata hivyo, ninaahidi kuandika pia kuhusu apps za jukwaa la iOS (Apple) kadri nitakavyokutana nazo. Tatizo kubwa linalonikwaza kuhusu apps za iOS ni ukweli kwamba mie nimekuwa mtumiaji wa Android kitambo sasa. Nilianza na HTC Desire kwa miaka miwili, kisha nikaja kwenye Samsung Galaxy S2 kwa miaka miwili tena, na sasa nipo na Samsung Galaxy S5 ambayo nina contract ya miaka miwili kutoka mwezi Machi mwaka huu. Vilevile ninatumia tablet ya Samsung Galaxy Tab2 10.1 kitambo sasa, na Tablet ninayofikira kuwa nayo huko mbeleni ni Samsung Galaxy Tab S 10.5 au nyingineyo ya Android.

Loe ninawaletea app moja inayoweza kukurahisishia kutuma SMS kutoka kwa kompyuta au tablet yako kwenda kwa simu yoyote ile.Sote twafahamu kuna nyakati twajikuta hatuna simu, na katika amzingira ya kawaida, huwezi kutuma SMS bila simu. Tatizo hilo lina ufumbuzi kwa kutumia apps mbalimbali, lakini ninayoipenda na kuitumia zaidi ni MIGHTY TEXT.

Cha kufanya ni kui-download kwenye simu yako, kisha kama una Tablet, download huko pia. Ili uweze kuitumia kwenye kompyuta yako, unapaswa kui-install kama extension ya browser ya Chrome au browser nyingine kama Safari, Firefox na Internet Explorer, kisha nenda kwenye app ya mtandaoni ya Might Text kwa ajili ya kuruhusu akaunti yako ya Google iiwezeshe app hiyo kutuma na kupokea SMS.

Iwapo utakumbana na tatizo lolote basi usisite kuwasiliana nami ili nikusaidie kupata ufumbuzi.

Endelea kutembelea blogu hii kupata habari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kama hii ya teknolojia, ambayo unaweza kuifikia kirahisi kwa kubonyeza TEKNOLOJIA kwenye menyu ya Blogu hii0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube