11 Aug 2014


WIKIENDI iliyopita haikuwa njema kwa mtangazaji Ephraim Kibonde baada ya kutupwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa msala wa kudaiwa kugonga gari na kutoa lugha ya matusi, Ijumaa Wikienda lina full stori.
Mtangazaji Ephraim Kibonde akidhibitiwa na Polisi wa usalama barabarani maeneo ya Mwenge.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho ambapo gari alilokuwa akilitumia Kibonde, liligonga kwa nyuma gari jingine na kisha kukimbia.
“Baada ya kugonga, Kibonde alirudi nyuma kisha kuanza kukimbia ambapo trafiki alitumia gari lililogongwa na Kibonde kumkimbiza,” kilimwaga data chanzo hicho.Chanzo hicho kilifafanua kuwa baada ya polisi kumkimbiza kwa saa kadhaa, walifanikiwa kumkamata maeneo ya Mwenge ambapo trafiki alipanda kwenye gari la Kibonde na kumuamuru arudi eneo la tukio lakini Kibonde hakuwa tayari kurudi ndipo alipoanza kukimbia tena, huku askari aliyemkamata akiwa ndani ya gari.
Ephraim Kibonde akiwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Inaonekana kulitokea kutoelewana kati ya askari na Kibonde ndipo askari huyo alipowasiliana na wenzie kwa njia ya radio call ili wambananishe na alipofika Ubungo kwenye mataa wakamtaiti na kumpeleka kituoni, Oysterbay,” kilihitimisha chanzo chetu.
Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alitia timu katika kituo cha Oysterbay ili kutaka kujua mustakabali mzima wa ishu hiyo ambapo alimshuhudia Kibonde akiwa amesimama nyuma ya nondo huku akiwa anaimba ‘nyimbo’ anazozijua mwenyewe.
Mtangazaji huyo amefunguliwa kesi iliyopewa RB namba OB/RB/13806/20014 KUGONGA NA   LUGHA YA MATUSI.


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.