Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,Mohamed Thabit Kombo akimpongeza Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel
kwa kuona jukumu la kusaidia jamii katika kuokoa maisha ya watoto njiti.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed
Thabit Kombo akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris
Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko huo,Doris Mollel akizungumza na wageni
waalikwa waliofika kwenye hafla ya kutambulisha Mfuko wa Doris
Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed
Thabit Kombo (pili kushoto),Balozi Mwanaid Maajar (kulia),Mwenyekiti wa Mfuko
huo,Doris Mollel (katikati) pamoja na wadau wengine wa Mfuko huo wakishiriki
kwa pamoja kukata keki,kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Doris
Mollel,uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wageni waalikwa katika hafla ya kutambulisha Mfuko wa
Doris Mollel,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhulia hafla hiyo.
Kutoka kulia ni HEENA ambaye ni mmoja kati ya washirika wakubwa wa mfuko
huo, wakiwa wameshikana mikono na muanzilishi wa mfuko huo miss DORIS MOLLEL
pamoja meneja wa mfuko huo RAHAB MBISE mara baada ya kuzindualiwa kwa mfuko huo
jijini Dar es samaam
Meneja wa mfuko huo RAHAB MBISE akizungumza wakati wa uzinduzi huo
uliofanyika jjini Dar es salaam
Mrembo wa singida aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya miss
tanzania mwaka wa 2014 DORIS MOLEL leo amezindua rasmi rasmi DORIS MOLEL
foundation ambayo ni mahususi kwa ajili ya kusaidia watoto ambao wamekuwa
wanazaliwa wakiwa bado hawajatimia NJITI ambapo amewataka watu mbalimbali
kujitokeza kumpa saport katika shighuli hiyo.
Uzinduzi huo ambao umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi pamoja na wadau wanaohusika katika kuwasaidia watoto hao. wengi
wamepongeza jitihada zinazoonyeshwa na mrembo huyo kwani watoto wanaozaliwa
wakiwa na tatizo hilo wamekuwa wakusahaulika sana nchini tanzania jambo ambalo
limetajwa kuwaadhiri watoto hao pamoja na wazazi wao.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mrembo DORIS ambaye ni mmoja kati ya watu walioathiriwa na
tatizo hilo (alizaliwa akiwa njiti) alisema kuwa
ameamua kuwasaidia watoto na wazazi wenye matatizo hayo baada ya yeye
kupitia katika kipindi kama hicho ambapo alisema kunahitajika msaada mkubwa
kutoka kwa watu wa mbalimbali.
“Mimi nilizaliwa nikiwa njiti nilikuwa sijafikisha uzito halali wa
kuzaliwa lakini nilizaliwa na mama akanisaidia hadi leo hii mnaniona hapa ni
miss Tanzania na ni mtu nayekubalika na jamii,hivyo nimeona kuna haja ya
kuwasaidia watoto kama mimi ambao wamezaliwa hivyo ili waweze kukua na afya
njema na baadaye kutimiza malengo ya maisha yao,”alisema mrembo huyo.
Alisema kuwa baada ya kuchaguliwa kuwa mrembo namba tatu wa Tanzania
alifikiria kitu cha kufanya ili arudishe shukrani kwa Watanzania na baada ya
kutembea katika maeneo mbalimbali aligundua kuwa watoto wanaokumbwa na matatizo
hayo bado wamekuwa hawapewi kipaumbele katika kusaidiwa jambo ambalo
limemsukuma yeye kuanza kufanya mchakato huo.
Aidha alisema kuwa ipo haja ya serikali pamoja na wadau mbalimbali kuunga
mkono jitihada hizo kwa lengo la kuokoa kizazi kikubwa ambacho kinazaliwa na matatizo
kama hayo ambapo kwa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto laki mbili
wanazaliwa wakiwa njiti kwa mwaka nchini Tanzania.
Uzinduzi huo uliambatana na uchangiaji wa mfuko huo kwa ajili ya
kuwasaidia watoto hao, ambapo watu mbalimbali wachangia na
kuwaomba Watanzania wengine kuendelea kumsaidia mrembo huyo kuhakikisha kuwa
anatimiza lengo lake.
Baadhi ya watu waliojitokeza kumpa nguvu katika shughuli hiyo leo ni
pamoja na muandaaji wa mashindani ya miss tanzania ambapo ndiko mrembo huyo
alikotokea bwana hashimu lundenga, Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) Mzee Iddi Simba, Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mohamed Thabit Kombo pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Bara na Viusiwani
0 comments:
Post a Comment