17 May 2016


"Hello world!" ndio ilikuwa tweet ya kwanza baada ya Idara ya ushushushu ya Uingereza inayohusika na kunasa mawasiliano, GCHQ (Government Communications Headquarters)  kujiunga na mtandao huo wa kijamii. 

Hawa jamaa, ambao makao yao makuu ni hayo pichani juu, ndio wenye jukumu la kusoma barua-pepe zetu, kusikia simu zetu na kutegesha vinasa sauti pale inapobidi, wamebobea kwenye hacking...kwa kifupi ukitaka kuwaelewa vema, m-Google yule jamaa anaitwa Edward Snowden..amewazungumzia vya kutosha, wao na washirika wao wa Marekani, wanaoitwa NSA.

Sasa hawa jamaa wameingia rasmi katika mtandao wa kijamii wa Twitter.Hiyo tweet yao ya kwanza ya "Hello world" iliyoambatana na picha ya ndani ya ofisi yao, ina umuhimu wa aina yake kwa sababu ni programu ya kwanza kujifunza kuandika wakati mtu anapojifunza kundika kwa lugha ya ku - code katika  vile Java, Python, C, PHP, na Ruby.

"Kwa kujiunga na mitandao ya kijamii, GCHQ inaweza kutumia sauti yake yenyewe kuongea  kuhusu kazi muhimu tunayofanya kuiweka Uingereza salama," alisema Andrew Pike, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa taasisi hiyo ya kishushushu.

Taasisi hiyo ya kishushushu imeeleza kuwa inataka kufikika (accessible) na kuufahamisha umma kuhusu shughuli zake. Kadhalika, inataka majadiliano na watu wenye ufahamu wa teknolojia hususan katika maeneo ya teknolojia, hisabati, usalama mtandaoni na mada nyinginezo.
1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube