11 Sept 2016

Tanzania yetu ipo katika msiba mkubwa (hata kama dalili za msiba hazionekane) kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jana alasiri kwenye eneo la ukanda wa Ziwa Viktoria, ambapo kwa mujibu wa taarifa, tetemeko hilo limepeleka vifo 13 hadi sasa na majeruhi takriban 200.Tetemeko hilo la ardhi lilikuwa na ukubwa (magnitude) wa kati ya 5.7 na 5.9 (taarifa bado zinakanganya) lilitikisa pia baadhi ya maeneo yanayozunguka Ziwa Victoria nchini Uganda na pia baadhi ya maeneo nchini Rwanda na kidogo nchini Kenya.

Picha ziliowekwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha uharibifu mkubwa katika mji wa Bukoba wenye wakazi takriban 70,000, sambamba na vifo na majeruhi.

"Tukio hili limesababisha maafa makubwa... kwa sasa hali imetulia..." alisema Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawila. "

Vipimo vya Idara ya Jiologia ya Marekani vinaonyesha kuwa tetemeko hilo la ardhi la kina cha kilomita 10 lilitokea saa 9.27 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Map showing Tanzania and Bukoba, where earthquake hit in September 2016
Bonde la Ufa la Afrika Mashariki linapita katika 'mstari wenye kasoro kijiolojia' (geologocal fault line), moja ya vyanzo vya matetemeko ya radhi duniani, lakini matukio ya matetemeko ya ardhi yamekuwa ni ya nadra.
Julai mwaka 2007, tetemeko la ardhi la 'magnitude' sita lilitokea Arusha, mkoa uliopo mashariki mwa Bukoba.

Kijiolojia, Bonde la Ufa la Afrika Mashariki linapita katika eneo kulikotokea tetemeko hilo la ardhi. Kwa kifupi, chanzo cha tetemeko hilo ni kutokana na tabaka la miamba katika eneo husika kuwa fukuto jingi la joto na kusigana kwa miamba, hali ambayo hupelekea miamba kukatika, na hiyo hupelekea ardhi itikisike.

Kwa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha matetemeko ya ardhi, BONYEZA HAPA 

MIMI BINAFSI NINATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA ZA MAREHEMU 13 WALIOFARIKI KUTOKANA NA TETEMEKO HILO, NA POLE KWA MAREJURHI TAKRIBAN 200. POLENI SANA WAFIWA NA NINAWAOMBEA MAJERUHI UPONYAJI WA HARAKA.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.