18 Sept 2016


Majuzi nilikutana na tweet ya rafiki yangu Profesa Kitila Mkumbo ambayo kidogo ilinitatiza. Mwanataaluma huyo ambaye ni pamoja na majukumu yake ya uhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni mshauri wa kitaalamu (consultant) wa taasisi ya Twaweza ambayo majuzi ilichapisha utafiti wake kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania.


Tweet ya Profesa Kitila iliyonigusa ni hii hapa chini
Tafsiri ya Kiswahili ni kwamba "tafiti za Twaweza zinawahoji Watanzania, sio tabaka la Watanzania wasomi pekee waliosheheni kwenye mitandao ya kijamii. Katika Tanzania, mitandao ya kijamii hairandani na dunia halisi."Kutokana na kuguswa kwangu, nilimjibu Profesa Kitila kama ifuatavyo


Nikimaanisha "inasikitisha pale watu wa tabaka halisi la wasomi kama wewe Profesa mnaposhindwa kutambua ni jinsi gani mitandao ya kijamii imebadilisha jinsi tunavyowasiliana."


Na Profesa 'akajitetea' kuwa anaelezea tu 'hali halisi,' na sio kama hathamini mitandao ya kijamii


Niliamua kuahirisha mjadala huo hadi siku nyingine licha ya ukweli kuwa siafikiani na mtazamo wa Profesa Kitila kwamba hali halisi ni kuwa mitandao ya kijamii hairandani na dunia halisi. Sawa, kuna vitu vingi/watu wengi feki katika mitandao ya kijamii, matajiri mtandaoni ilhali masikini wa kutupwa katika maisha yao halisi, furaha mitandaoni lakini majonzi katika maisha halisi, na vitu kama hivyo.

Hata hivyo, miongoni mwa vitu chanya kuhusu mitandao ya jamii ni katika jinsi inavyorahisisha maisha yetu. Na katika hili sio kwa tabaka la wasomi pekee bali takriban kila mtu mwenye uwezo wa kutumia inteneti. 

Na kama kuna kundi ambalo bado linasuasua katika matumizi ya mitandao ya kijamii hukoTanzania basi ni hilo la wasomi. Wakati kwa huku nchi za Magharibi ni suala la kawaida kwa watu wa tabaka la juu kuwasiliana na wenzao wa tabaka hilo au hata wa tabaka la chini kwa meseji, iwe SMS au Whatsapp, kwetu sie 'vigogo' wengi bado wana 'fikra za mwaka 47' kwamba kumtumia mtu meseji ni kama 'mtu amefulia, hana uwezo wa kupiga simu.'

Enewei, lengo la makala hii sio kuelezea kuhusu mjadala huo mfupi kati yangu na Profesa Kitila bali kutoa darasa kuhusu namna ya kurekodi call ya whatsapp na jinsi ya ku-share na ku-save voicenote ya Whatsapp.

Kwanini darasa hili ni muhimu? Kwa sababu Whatsapp imekuwa mkombozi wetu mkubwa katika kukwepa gharama za mawasiliano hususan kwa sie tunaofanya mawasiliano ya kimataifa.

Na kwanini unaweza kuhitaji kurekodi Whatsapp call? Well, labda ni kwa sababu unahitaji kuisikia call hiyo baadaye, lakini pia pengine kuna mtu anakubighudhi na wahitaji kumrekodi kwa minajili ya kumchukulia hatua za kisheria.

KUREKODI WHATSAPP CALL

Katika mazingira ya kawaida, Whatsapp hurekodi calls zote na kuzihifadhi kwenye SD card katika folder liitwalo "Whatsapp calls."
Record WhatsApp Calls
Record WhatsApp Calls
Lakini uwepo wa faili hilo unategemea aina ya simu unayotumia, na iwapo simu yako ina SD card. Na kuna nyakati folder hiyo ipo lakini haina kitu ndani yake.

Kadhalika, inaelezwa kuwa hata kama kuna mafaili yenye calls kwenye folder hiyo, basi calls hizo zina sauti yako tu na sio zote, yaani yako na mtu unayeongea nae.

Kutatua tatizo hilo inabidi kutumia apps zinazorekodi calls. Type 'whatsapp call recorder' na utakutana na orodha ya apps kadhaa. Ushauri wangu ni kwamba jaribu apps mbalimbali kabla hujaamua ipi ni bora zaidi kwa mahitaji yako. 

Mie natumia Samsung Galaxy Note 4 (usipoteze fedha zako ku-upgrade to aidha Note 5 au Note 7 kwani Note bora kabisa ni Note 3 na Note 4, hizo nyingine ni mbwembwe tu. Nitaelezea kuhusu hilo katika makala nyingine) na app ninayotumia kwa kurekodi calls za Whatsapp ni All Call Recorder. 

Kuhusu ku-save au ku-share voice notes za Whatsapp, maelekezo ni rahisi tu. 

1. Highlight voicenote husika kisha click share
2. Share hiyo voice note kwa app inayoweza kuipeleka kwa computer yako. Mie natumia aidha 'Send Anywhere' au 'Pushbullet.'
3. Ukishafikisha kwa computer yako, hatua inayofuatia ni kwenda kwenye website hii www.online-covert.com kisha upload voice yako ambayo itakuwa kwenye mfumo wa faili la sauti wa .opus
4. Ili ku-upload, chagua sehemu iliyoandikwa 'Audio converter.' Kisha kwenye drop-down menu (pameandikwa 'select target format') chagua 'covert to mp3' kisha click 'go.'
5. Utapelekwa kwenye ukurasa mwingine ambapo unatakiwa kwenda palipoandikwa ' upload your audio you want to convert to mp3' kisha bonyeza 'choose your file' itakupeleka mahala ulipohifadhi voice note yako ya Whatsapp kwenye computer yako ikiwa katika mfumo wa faili la sauti wa .opus
6.Upload kisha nenda palipoandikwa 'convert file' katika tovuti hiyo ya www.online-covert.com
7. Ikishamaliza kubadili mfumo wa file la sauti kutoka .opus ya whatsapp voice note kwenda mp3, file husika litakuwa downloaded tayari kwa matumizi yako mengine

Ukitaka ku-save voice note ya Whatsapp, 
1. Highligh voice note husika
2. Chagua share pale juu ya whatsapp
3 Chagua app unayotaka kutumia ku-share
4. Peleka voice note hiyo kwenye app ya ku-save mafaili, zilizo maarufu zaidi ni Google Drive, Dropbox au One Drive. Chaguo ni lako.

Kama una swali au maoni au hata kukosoa basi usisite kunitumia kupitia sehemu ya 'comment.' Endelea kutembelea blogu hii kwa habari mbalimbali za teknolojia na nyinginezo. Karibuni sana 0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube