9 Dec 2016

Leo ni siku ya Uhuru wa nchi yetu, tunatimiza miaka 55 kama taifa huru. Siku kama ya leo, miaka 55 iliyopita, Tanganyika ilikabidhiwa uhuru wake kutoka kwa Mwingereza. Japo kuna wanaohoji iwapo tupo huru kweli, kwa leo tusherehekee tukio hilo la mkoloni kutukabidhi nchi yetu.

Pia siku ya leo ni siku yangu ya kuzaliwa. Ninamshukuru Mungu kwa kila kitu. 


Ninawashukuru pia wazazi wangu ambao japo ni marehemu kwa sasa, kiroho nipo nao siku zote: marehemu baba Mzee Philemon Chahali na marehemu mama Adelina Mapango. Bwana Mungu awajalie pumziko la milele na mwanga wa milele awaangazie mpumzike kwa amni. Amen. Naishukuru familia yangu hasa dadangu Sr Maria-Solana Chahali na wadogo zangu mapacha Peter (Kulwa) na Paul (Doto). Naomba Bwana Mungu atujalie maisha marefu zaidi, afya njema na mafanikio katika shughuli zetu za kila siku.

Katika maadhimisho haya ya siku yangu ya kuzaliwa, ninatoa zawadi ya kopi za bure za kitabu changu hicho pichani chini.BONYEZA HAPA kuki-download BURE

1 comment:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.