Showing posts with label HIGHER EDUCATION. Show all posts
Showing posts with label HIGHER EDUCATION. Show all posts

13 May 2008

Niliposikia mara ya kwanza nilidhani ni stori tu za mjini.Jana nimesikia tena,na safari hii ni kutoka kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita hivi majuzi.Ishu yenyewe iko hivi:eti wanafunzi wa kidato cha sita waliletewa mashuleni fomu za kuomba udhamini wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Hadi hapo hakuna tatizo,Bodi inawajali wanafunzi hai inawaletea fomu shuleni.Mgogoro unaanzia kwenye taratibu za kurejesha fomu hizo ambapo kila mwanafunzi alipaswa kulipia shs 10,000/= ambazo ni non-refundable.Mgogoro zaidi ni ukweli kwamba zoezi zima la kujaza na kurejesha fomu hizo lilifanyika hata kabla wanafunzi hao hawajafahamu matokeo yao.Kwa maana hiyo,mwenye kufaulu na kufanikiwa kupata admission ya chuo anakuwa amenufaika lakini kwa aliyepata maksi zisizomruhusu kuendelea na masomo ndio ameliwa.This is what we call daylight robbery.Kwanini wasingechukua hiyo elfu 10 baada ya matokeo ili wale wasio na sifa wasiliwe fedha zao bure?Deadline ya kurejesha fomu hizo ilikuwa tarehe 30/04 na matokeo ndio yametoka majuzi.Sipendi kuona mikopo ya wanafunzi inageuzwa kuwa kama bahati nasibu flani,or to be more precise,ujambazi wa mchana kweupe.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.