Showing posts with label NEW MOUNT MERU HOTEL. Show all posts
Showing posts with label NEW MOUNT MERU HOTEL. Show all posts

2 Dec 2010



Nimetumiwa na mdau,nami nawasilisha

Nadhani kwa wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake watakuwa wameshaona kwenye mabango mbalimbali barabarani ama kupitia redio ama magazeti ya kuwa iliyokuwa inaitwa Novotel Mount Meru Hotel inafunguliwa tena upya ikijulikana kama New Mount Meru Hotel.

Kikubwa nachotaka kuwafikishia watanzania wenzangu ni kuwa nimestaajabika sana ile maana kamili ya uwekezaji kuendelea kutupwa kapuni. Huwezi amini moderator na watanzania kwa ujumla, Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.

Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??

Kali zaidi ni kuwa Senior staffs woote ni ndani ya sauzi afrika ama asia au kwa watani wa jadi, ina maana hapa hatuna mameneja wazuri wakuendesha hotel? hatuna mashefu wazuri hapa tz?

Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??

Kama uwekezaji ndo hivi jamani bora tufie na tai shingoni.

Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17 Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then Mkapa na Magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??


Ama ndio kichwa cha mwendawazimu??


TUAMKE WATANZANIA NA TULIANGALIE HILI SWALA LA MOUNT MERU KWA JICHO LATATU.


NGUVU YA UMAA IFANYE KAZI JAMANI............

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.