Showing posts with label NIC. Show all posts
Showing posts with label NIC. Show all posts

16 May 2009


MSIKIE MATTAKA ANAVYOONGEA KWA KUJIAMINI KANA KWAMBA ALIJITEUA MWENYEWE KUWA MKURUGENZI WA ATCL NA KUJIPA UJUMBE WA NIC.


Mattaka ajiweka kando ATCL
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 16th May 2009

Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL),
David Mattaka ametangaza kutoiongoza kampuni hiyo kwa miezi sita kutokana na kuteuliwa kuwamiongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Katika taarifa ya barua hiyo iliyotolewa na ofisi yake kwa wafanyakazi Mei 11, mwaka huu, inaonyesha kuwa Mattaka amelazimikakutofanya kazi ATCL kwa kipindi hicho kutokana na nafasi yake hiyo aliyoteuliwa naWaziri wa Fedha na Uchumi, Aprili 23, mwaka huu kuwamo katika Bodi ya Wakurugenzi ya NIC kazi ambayo zinamtaka awapo wakati wote kazini.

Uteuzi huo sambamba na wa Rais Jakaya Kikwete wa Februari 23, mwaka huu wa kuwamo katika kikosikazi cha kulifufua shirika hilo, Mattaka alisema “Katika nafasi zote nilizoteuliwa zinanitaka nifanye kazi muda wote kuanzia Mei mosi.” Kutokana na nafasi hizo mpya, kwa kipindi cha miezi sita ambayo hatakuwao ATCL, Bodi ya Wakurugenzi imemteua William Haji kukaimu nafasi yake.

“Bodi ya Wakurugenzi imemteua William Haji kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na CEO kuanzia Mei 8 na wakati huohuo kuendelea na nafasi yake ya Mkurugenzi wa Fedha,” alisema Mattaka. Bodi ya Wakurugenzi ya NIC iliyoanza kazi Mei mosi, inaongozwa na Mwenyekiti Balozi Charles Mutalemwa na wajumbe ni Michael Mhando kutoka Bima ya Afya, Msajili wa Hazina Agnes Bukuku, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kate Bandawe na Charles Kilasile.

CHANZO: Habari Leo

KWA UPANDE FLANI,HATUWEZI KUMLAUMU KWANI KWA HAKIKA ALIYEMTEUA AMEONEKANA KURIDHISHWA NA UTENDAJI WAKE.USHKAJI KATIKA TEUZI NI MIONGONI MWA VYANZO VIKUU VYA KUSUASUA NA HATIMAYE VIFO VYA TAASISI MBALIMBALI ZA UAMMA,BILA KUSAHAU KUSHAMIRI KWA UFISADI.KWANI HAKUNA WATU WENYE UWEZO ZAIDI YA MATTAKA?KAMA AMECHEMSHA ATCL,ATALETA MIUJIZA GANI HUKO BIMA?


YANI TUNAVYOENDESHA MAMBO KIHOLELA UTADHANI TUSHAPIGA HATUA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KUMBE WAPI.VICHWA VILIVYOISHIWA MAWAZO NA MBINU ZA KUNUSURU TAASISI ZA UMMA HAVIWEZI KULETA MAPYA YOYOTE VINAVYOZUNGUSHWA KIUSHKAJI KUTOKA TAASIS MOJA KWENDA NYINGINE KANA KWAMBA NI ZA KIFAMILIA.Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube