Showing posts with label PADRE KARUGENDO. Show all posts
Showing posts with label PADRE KARUGENDO. Show all posts

7 Jan 2009

Padre Privatus Karugendo amekuwa akisimulia mkasa ulisababisha yeye kusimamishwa,na hatimaye kuvuliwa,daraja la upadre.Kma nilivyoeleza katika post hii,japo sifahamiani personally na Mtumishi huyu wa Bwana,alikuwa columnist mwenzangu katika jarida la Raia Mwema hadi nilipolazimika kuchukua "sabbatical leave" ya uandishi wa makala.Pia,maandiko mbalimbali ya Padre Karugendo yalinipa changamoto kubwa hadi nikaamua kujiingiza katika anga za uandishi wa makala kwenye magazeti mbalimbali huko nyumbani.

Unaweza kusoma SIMULIZI kuhusu chanzo cha mkasa uliopelekea Padre huyo kusimamishwa na hatimaye kuvuliwa upadre kwa KUBONYEZA HAPA (Sehemu ya Kwanza) na HAPA (Sehemu ya Pili) na HAPA (latest).Blogu hii itaendelea kuwaletea simulizi hizo kadri zinavyochapishwa gazetini.Mkasa uliomkumba Padre huyu unanigusa sio tu kwa vile napenda makala zake au kwa sababu tuliwahi kuandikia gazeti moja,bali pia kwa vile kwa namna flani yeye,kama mie,ni majiruhi wa mfumo uliozowea kupongezwa na kunyenyekewa lakini usiotaka kusikia criticism au mawazo mbadala.
NYONGEZA: Nimekutana na post katika blogu ya Pambazuko ambapo Askofu (anayetajwa kwenye Simulizi za Karugendo) ANADAIWA KUWA NA MTOTO NA ANATAKIWA AKAMCHUKUE. (Bonyeza link kuisoma)

6 Jan 2009

Picha kwa hisani ya Mjengwa.

Habari hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la  Sunday Citizen.Pia,mwanablogu BWAYA ameichambua kwa undani habari hiyo ya kusikitisha.Makala za Padre Karugendo ni miongoni mwa maandiko yaliyonishawishi nami njiingize kwenye fani ya uandishi wa makala.Nahisi Kanisa Katoliki limechukua hatua hiyo kutokana na msimamo makini na wa uwazi wa Padre Karugendo kuhusiana na mambo mbalimbali ya Kanisa hilo.Japo mie ni Mkatoliki pia,lakini sipendezwi na namna Kanisa hili lisivyopenda kukosolewa.Nalinganisha tukio hili na lie la Father Nkwera (na wanamaombi) ambaye kimsingi kosa lake kubwa ni kutumia karama kama ile aloyokuwanayo Bwana Yesu ya kuponyesha wagonjwa.Yayumkinika kubashiri kwamba hatma ya Kanisa letu sio ya kuleta matumaini sana kama litaendeleza UKALE na kujifanya halitambua dunia inavyobadilika.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.