Kwa lugha za Mlimani (UDSM) kilaza ni mtu ambaye shule haipandi.Kwake siku ya seminar presentation ni kama kutoa ushahidi kwenye kesi mahakamani ambayo inaweza kumpelekea kunyongwa.Ratiba ya mtihani ikitoka basi kwake inakuwa kama amepewa ratiba ya kifo chake.Vilaza huwa makini sana katika kuchagua marafiki chuoni hapo,hujitahidi kujiweka karibu na vipanga (kinyume cha vilaza).Kipanga halisi anaweza kuonekana kwenye lectures kwa msimu,muda mwingi anautumia kwa shughuli zake binafsi,na si ajabu kumkuta anakamata kinywaji pale Duso wakati watu wanahangaika library.Ni nadra kuwaona vipanga halisi kwenye discussion groups.Lakini come the UE,vipanga wanaendelea kutesa.Well,hiyo ni Mlimani niliyoiacha 1999.Sijui mambo yakoje kwa sasa.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanamtuhumu Sarah Palin,mgombea mwenza wa John McCain, kuwa huenda ni kilaza na ndio maana amekuwa akikwepa mahojiano ya maana na vyombo vya habari.Zaidi SOMA HAPA